UTI
• • • •
MASWALI NA MAJIBU KUHUSU UGONJWA WA UTI(karibu darasa afya)
SWALI 1: Hivi mtu anaweza kupata maambukizi ya UTI kwa kunywa maji machafu?
MAJIBU; Ugonjwa wa uti ambapo kirefu chake ni urinary track infection,ni ugonjwa ambao huathiri mfumo mzima wa mkojo, hivo ni mashambulizi ya vimelea vya magonjwa kama vile Bacteria kwenye mfumo mzima wa mkojo mfano; Njia ya mkojo, kibofu cha mkojo, figo, tezi la Prostate N.K
SWALI 2: Maana ya UTI ni nini?
MAJIBU; UTI ni kifupi cha maneno ya kingereza yaani urinary track infection,huku ikiwa na maana ya maambukizi katika mfumo mzima wa mkojo kama nilivyokwisha kueleza hapo juu
SWALI 3: Zipi ni dalili za ugonjwa wa UTI kwa mwanaume na mwanamke?
MAJIBU; Dalili za ugonjwa wa UTI kwa mwanaume na mwanamke ni pamoja na
- Maumivu makali wakati wa kukojoa
- Kuhisi hali ya kuchomwa na mkojo wakati wa kukojoa
- Kukojoa mara kwa mara
- Kutoa mkojo wenye harufu kali na ambao umebadilika rangi kwa wakati mwingine
- Kupatwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu au pembeni kidgo hasa hasa upande wa kushoto
- Kwa mwanamke huweza kupatwa na hali ya kukauka sehemu za siri au ukeni pamoja na kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
N.K
SWALI 4: Je Dawa ya kutibu UTI ni dawa gani?
MAJIBU; Matibabu ya Ugonjwa wa Uti huhusisha dawa nyingi lakini miongoni mwa dawa hizo ni pamoja na; Ciproflaxin, Azuma(azthrimycin), Amoxicillin N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!