MATUMIZI YA ASALI KUTIBU VIDONDA(asali ni dawa nzuri sana)

 ASALI NA VIDONDA

• • • • • •

MATUMIZI YA ASALI KUTIBU VIDONDA(asali ni dawa nzuri sana)


Asali ni dawa kubwa ya kusaidia mtu mwenye vidonda mbali mbali. Hapa tunazungumzia kila aina ya kidonda mfano; vidonda vya tumbo, vidonda vinavyotokana na kuungua,Malengelenge,majeraha ya kuanguka,ajali za gari,pikipiki,kuchomwa na vitu vya ncha kali kama vile; kisu,mabati,misumari,chupa N.K


FAIDA ZA ASALI KWENYE KUTIBU VIDONDA MBALI MBALI NI PAMOJA NA;


1. Kusaidia kuondoa harufu mbaya inayotoka kwenye kidonda. Matumizi ya asali huweza kukata kabsa harufu mbaya kutoka kwa kidonda.


2. Kusaidia kukausha unyevu wote kwenye kidonda na kutengeneza mazingira magumu kwa bacteria kuweza kushambulia kidonda hicho. Kwani bacteria hupenda mazingira ya unyevu unyevu.


3. Kusaidia vidonda kupona kwa haraka zaidi. 


4. Ndani ya asali kuna virutubisho mbali mbali ambavyo ni muhimu sana kwenye afya ya Ngozi pamoja na kuponesha ngozi kwa haraka zaidi.



TAHADHARI; Ni vizuri kutumia asali baada ya uchunguzi wa kina wa kidonda chako pamoja na kupewa maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya. Na ndipo wakiona inafaaa kutumia asali kwa kidonda chako basi unaweza kupata faida za matumizi haya ya asali.


-


Hakikisha unapaka asali kwenye kidonda safi baada ya kusafishwa,sio unapaka juu ya uchafu


-


KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!