MATUMIZI YA CONDOM KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO(faida na hasara zake)

 CONDOM

• • • • •

MATUMIZI YA CONDOM KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO(faida na hasara zake)


Hii ni mojawapo ya njia ambazo hutumiwa na watu wengi kwa malengo mbali mbali, Na njia hii huweza kutumiwa na watu wa jinsia zote mbili, nikiwa na maana kwamba,kuna condom za kiume na kuna condom za kike pia.


FAIDA ZA MATUMIZI YA CONDOM KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO


- Ni mojawapo ya njia nzuri ya kupanga uzazi ambayo ni rahisi kutumia


- Ni njia ya uzazi wa mpango isiyo na kichocheo chochote,hivo kumuepusha mtumiaji na madhara mbali mbali kama vile mvurugiko wa vichocheo mwilini N.K, Kama ilivyo kwa njia nyingine za kupanga uzazi mfano Sindano


- Condom pia husaidia kukukinga na magonjwa mengine mbali mbali ya zinaa kama vile,kaswende,kisonono, Ukimwi n.k Tofauti na njia zingine za kupanga uzazi


HASARA ZA KUTUMIA CONDOM KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO


- Ni rahisi kupitiwa na kuacha kutumia kila mara,kitu ambacho huleta hatari ya kupata mimba zisizotarajiwa yaani unplanned pregnancy


- Shida ya kubeba kila mahali unapokwenda tofauti na njia nyingine kama kipandikizi


- Pia, isipotumiwa vizuri kwa uangalifu mkubwa,huweza kupasuka na kupelekea kupata mimba zisizotarajiwa


- Kuna baadhi ya watu husema,condom hupunguza ladha ya mapenzi, hii ni kutokana na kukosekana kwa mgusano wa ngozi kwa ngozi pamoja na kukosa joto halisi wakati wa tendo la ndoa.


-


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!