MAUMIVU MAKALI YA KICHWA HUSABABISHWA NA NINI?

 KICHWA

• • • • •

MAUMIVU MAKALI YA KICHWA HUSABABISHWA NA NINI?


Nidhahiri kwamba katika maisha yetu hakuna mtu ambaye hajawahi kuumwa na kichwa  japo maumivu haya ya kichwa huweza kutofautiana kati ya mtu na mtu, ikiwa ni pamoja na ukubwa wa maumivu pamoja na sehemu ya kichwa ambapo mtu huhisi maumivu ya kichwa,Mfano; mwingine huhisi maumivu ya kichwa kwa mbele,mwingine huhusi maumivu ya kichwa kwa pembeni N.K.


CHANZO CHA TATIZO LA MAUMIVU MAKALI YA KICHWA


Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mtu kupatwa na maumivu makali ya kichwa, na sababu hizo ni pamoja na;


1. Mtu kuwa na msongo wa mawazo, pale ambapo umewaza jambo flani kwa mda mrefu au kwa kina sana huweza kukusababishia hali ya kuumwa na kichwa sanaa.


2. Mtu Kuumwa na kichwa huweza kuwa dalili ya magonjwa mbali mbali, kama vile Ugonjwa wa Malaria,UTI, N.K, hivo maumivu makali ya kichwa huweza kutokea pale ambapo tayari mtu ana ugonjwa Flani.


3. Maumivu makali ya kichwa huweza kusababishwa na Uchovu sana wa mwili,endapo mtu amechoka sana ikiwa ni kutokana na sababu mbali mbali kama kazi nzito za siku husika,basi huweza kupatwa na tatizo la kuumwa sana na kichwa.


4. Matumizi ya baadhi ya Njia za uzazi wa mpango,ifahamike kwamba moja ya maudhi madogo madogo au tunasema Side Effects ambazo mwanamke huweza kuzipata baada ya kutumia Njia za uzazi wa mpango kama vile Sindano, Vipandikizi N.K ni pamoja na kupata maumivu makali ya kichwa mara kwa mara.



5. Mtu kuwa na kiwango kikubwa cha damu mwilini, hali hii huweza kukufanya uwe na tatizo la maumivu makali ya kichwa ambayo kwa wakati mwingine huweza kuambatana na kizunguzungu kikali.


6. Tatizo la Presha, ikiwa ni pamoja na Ugonjwa wa presha ya macho au Glaucoma ,huweza kusababisha shida ya maumivu makali ya kichwa kwa baadhi ya wagonjwa.


7. Maumivu makali ya kichwa kwa wanawake wakati wakiwa kwenye Hedhi, Wapo baadhi ya wanawake wakiwa kwenye kipindi cha hedhi(au siku zao) hupata maumivu makali sana ya kichwa, huku wengine maumivu hayo yakiambatana na Homa au hali ya joto la mwili kuwa juu.


NINI KIFANYIKE BAADA YA WEWE KUWA NA MAUMIVU MAKALI YA KICHWA?


- Huduma ya kwanza kwako, ni pamoja na kunywa maji mengi ya kutosha.


- Endapo tatizo bado lipo unaweza kwenda hosptal ili kuongea na wataalam wa afya na kupewa dawa sahihi kwako baada ya kujua chanzo cha tatizo lako. Miongoni mwa dawa ambazo husaidia sana maumivu ya kichwa ni pamoja na Paracetum au Panadol.


- Epuka matumizi ya hovio ya dawa kabla ya kujua chanzo cha tatizo lako



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!