MBINU ZA KUONGEZA KINGA YA MWILI(kwa kitaalam hujulikana kama Immunity system booster)

 KINGA YA MWILI

• • • • • •

MBINU ZA KUONGEZA KINGA YA MWILI(kwa kitaalam hujulikana kama Immunity system booster)


Ifahamike kwamba hakuna ulizi na usalama wa mwili wa binadamu pasipo kinga ya mwili, Mfumo wa Kinga ya mwili maarufu kama Body Immunity sytem ndyo hupambana na kila aina ya mashambulizi kama vile magonjwa na kuhakikisha mwili wako unakuwa salama kila siku na kuendelea kufurahia maisha.


MBINU ZA KUONGEZA KINGA YA MWILI NI PAMOJA NA;


1. Punguza na dhibiti kadri uwezavyo kiwango cha hofu, mashaka na waswas. Tafiti zinaonyesha kwamba moja ya vitu vikubwa ambavyo hushusha kinga ya mwili wako kwa haraka zaidi ni pamoja na kuwa na Hofu kubwa. Ondoa na dhibiti hali hii hasa hasa kwakufanya vitu mbali mbali kama mazoezi, kujichanganya na watu na kuongea mambo mbali mbali ya kufurahisha, N.K


2. Jitahidi kufanya mazoezi kila siku. Moja ya vtu vikubwa ambavyo husaidia kujenga kinga Imara ya mwili ni pamoja na kufanya mazoezi kila siku. Hata wewe utakuwa shahidi wa hili,ni kwanini watu wanaofanya mazoezi hawaugui ugui magonjwa? .Nafikiri majibu utakuwa umeyapata. Kwamba kinga yao ya mwili ni imara na sio rahisi kushambuliwa  na magonjwa mbali mbali.


3. Hakikisha unapata muda wa kutosha wa kulala.  Tafiti zinaonyesha kwamba watu ambao hawapati muda wa kutosha wa kulala hupatwa na magonjwa kwa urahisi kuliko wale wanaopata muda mzuri wa kulala, Hivo kulala muda wa kutosha kiafya ni vizuri na huimarisha kinga yako ya mwili.


4. Pendelea kula vyakula jamii ya mimea,mfano mboga za majani, karanga, mafuta yaAlzeti N.K. Ndani ya vyakula hivi kuna ANTIOXIDANTS ambazo husaidia kumkinga mlaji na vimelea hatari vya magonjwa.


5. Hakikisha unakunywa maji ya kutosha kwa masaa 24. Kwa wastani angalau unywe lita 2.5 mpaka 3 Kwa siku. Huwa husaidia sana mwili wako kuwa vzr na kinga ya mwili kufanya kazi kwa ubora zaidi.


6. Epuka matumizi ya vitu ambavyo vina kemikali mbali mbali, kwani huweza kudhoofisha kinga yako ya mwili kwa urahisi zaidi.


-


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!