AFYA YA NGOZI
• • • • •
MBINU ZA KUTUNZA NGOZI YAKO YA MWILI(ijue afya ya ngozi)
Katika kutunza ngozi ya mwili na kuleta afya ya ngozi,wanawake wameonekana kujali sana hili na kujaribu mbinu mbali mbali ili kuhakikisha ngozi inakuwa safi na laini. japo kuna mambo pia wanayafanya bila kujua athari zake kwenye ngozi pamoja na mwili mzima.
VITU VYA KUZINGATIA ILI KULETA AFYA YA NGOZI PAMOJA NA USALAMA WAKE
1. Epuka matumizi ya vipodozi ambavyo vina kemikali ambazo zitaharibu uimara wa ngozi yako, kama vile zenye kemikali za hydrogen perixode.
2. Kumbuka ngozi yako hufanya kazi nyingi ikiwemo ya ulinzi dhidi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa hivo itunze sana.
3. Zingatia pia katika aina za sabuni unazotumia kuogea na kusafisha ngozi ya mwili wako,kwani sabuni zingine sio salama kwako.
4. Zingatia mafuta,Poda na vitu vingine unavyopaka ngozi yako,kwani vingine sio salama kwa afya ya Ngozi
5. Tunda la parachichi limeonekana kwa kiasi kikubwa kusaidia katika afya ya Ngozi. Hivo pendelea kutumia tunda la parachichi mara kwa mara.
6. Mionzi ya jua ikiwa mikali huweza kuathiri muonekano wa ngozi,wewe ni shahidi baadhi ya watu wakichomwa sana na jua ngozi ya mwili huwa nyekundu hasa hasa watu weupe.
-
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!