MWANAMKE SHUPAVU NI YUPI KATIKA NYANJA YA AFYA?

 MWANAMKE

• • • • • •

MWANAMKE SHUPAVU NI YUPI KATIKA NYANJA YA AFYA?


1. Mwanamke shupavu ni yule ambaye akihisi dalili yoyote ya magonjwa hukimbilia hosptal na kuongea na wataalam wa afya.


2. Mwanamke shupavu ni yule ambaye akipewa dawa za kuongeza damu wakati wa ujauzito maarufu kama FEFOL au vidonge vya FOLIC ACID huvitumia kama alivyoelekezwa na wataalam wa afya na sio kuvificha au kuvitupa.


3. Mwanamke shupavu ni yule ambaye hana tabia ya kutumia dawa hovio pale anapohisi mgonjwa bila maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya.


4. Mwanamke shupavu ni yule ambaye huweza kumshawishi mume wake umuhimu wa wote wawili kuhudhuria kliniki kipindi cha Ujauzito.


5. Mwanamke shupavu ni yule ambaye huchomwa sindano zote tano za kuzuia tetenasi .


6. Mwanamke shupavu ni yule ambaye ameshapata chanjo ya kuzuia ugonjwa wa homa ya ini maarufu kama Hepatitis B vaccine.


7. Mwanamke shupavu ni yule ambaye hupima maambukizi ya virusi vya ukimwi mara kwa mara


8. Mwanamke shupavu ni yule ambaye kama ana Virusi vya ukimwi hutumia dawa zote kutokana na maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya.


 9. Mwanamke shupavu ni yule ambaye baada ya kujifungua humnyonyesha mtoto ndani ya miezi sita maziwa yake pekee bila kumchanganyia mtoto na vyakula vingine.


10. Mwanamke shupavu ni yule ambaye anahakikisha mtoto wake ananyonya ndani ya miaka miwili au mitatu.


11. Mwanamke shupavu ni yule ambaye anahudhuria kliniki akiwa mjamzito.


12. Mwanamke shupavu ni yule ambaye humpeleka mtoto wake kliniki zote kama inavyotakiwa kwa mtoto baada ya kuzaliwa na mpaka  kufikisha umri wa miaka mitano.


13. Mwanamke shupavu ni yule ambaye humkumbusha mume wake matumizi ya dawa zozote ambazo amepewa maelekezo na wataalam wa afya kama ni mgonjwa.



14. Mwanamke shupavu ni yule ambaye anahikikisha anajua dalili zote za magonjwa muhimu kwa wanawake ambayo yanahitaji msaada wa haraka kama vile; Kansa ya matiti,kansa ya kizazi au kansa ya shingo ya kizazi,tatizo la uvimbe wa kizazi N.K


15. Mwanamke shupavu ni yule ambaye anatabia ya kufanya full checkup ya mwili wake mara kwa mara ili kuweza kugundua mapema endapo atakuwa na tatizo lolote ka kiafya.


16. Mwanamke shupavu ni yule ambaye huhudhuria kliniki zote pindi akiwa mjamzito.


17. Mwanamke shupavu ni yule ambaye hanywi pombe wala kuvuta sigara wakati akiwa mjamzito.


18. Mwanamke shupavu ni yule ambaye anaelewa jinsi ya kujichunguza mwenyewe saratani ya matiti hata akiwa nyumbani.


19. Mwanamke shupavu ni yule ambaye anajua maandilizi yote ya kujifungua na kujiandaa pindi akiwa mjamzito.


20. Mwanamke shupavu ni yule ambaye anafanya mazoezi ya mwili,ili kuweka mwili wake sawa na kuongeza kinga ya kupambana na magonjwa mbali mbali.






0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!