NAPATA MAUMIVU MAKALI YA TUMBO NA NYONGA JE SHIDA NI NINI?(swali la siku)

 AFYA TIPS

• • • •

NAPATA MAUMIVU MAKALI YA TUMBO NA NYONGA JE SHIDA NI NINI?(swali la siku)


MAJIBU; Tatizo hili huwapata watu wengi kwa hivi sasa na zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia uwepo wa shida hii kama vile;


- Kupatwa na maambukizi katika mfumo wa mkojo yaani UTI ambapo unaweza kupata maumivu ya tumbo hasa usawa wa kitovu au chini ya kitovu kidogo upande wa kushoto pamoja na maumivu ya kiuno na mgongo.


- Kupatwa na tatizo la appendix au kidole tumbo, ambapo moja ya dalili zake kubwa ni kupata maumivu makali ya tumbo usawa wa kitovu kuelekea upande wa kulia.


- Kufanya kazi za kuinama au kukaa kwa muda mrefu huweza kukuletea maumivu makali ya nyonga


- Kwa mwanamke, maumivu makali ya tumbo huweza kutokea kipindi cha hedhi


- Kwa mwanamke, huweza kupata maumivu makali ya nyonga,mgongo na tumbo kutokana na maambukizi katika via vyake vya uzazi yaani PELVIC INFLAMMATORY DISEASE(PID)


- Kupatwa na tatizo la homa ya matumbo au typhoid huweza kusababisha maumivu ya tumbo


- Hata tatizo la fangasi sehemu za siri hasa kwa wanawake huweza kusababisha maumivu makali ya tumbo


- Magonjwa mbali mbali ya zinaa kama kaswende,kisonono Chlamydia N.K


- Homa ya uti wa mgongo huweza kuleta maumivu makali eneo lote la nyonga pamoja na mgongo


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!