NJIA YA UZAZI WA MPANGO AINA YA KITANZI AU LUPU(inafanyaje kazi,faida na madhara yake)
KITANZI(LUPU)
• • • • •
NJIA YA UZAZI WA MPANGO AINA YA KITANZI AU LUPU(inafanyaje kazi,faida na madhara yake)
Miongoni mwa njia za uzazi wa mpango ambazo hushauriwa na wataalam wa afya katika matumizi ni pamoja na njia hii ya kitanzi au lupu. Njia hii ina uwezo wa kuzuia mimba kwa kipindi cha miaka 10 mpaka 12.
Njia hii hufanya kazi kwa kuzuia mbegu ya mwanaume kukutana na yai la mwanamke hivo kutokuwa na uwezekano wa urutubishaji kutokea na mimba kushika.
FAIDA ZA MATUMIZI YA KITANZI AU LUPU KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO
1. Ni njia ya muda mrefu katika kupanga uzazi
2. Njia hii haina aina ya kichocheo chochote hivo ni salama zaidi kwa mtumiaji
3. Njia hii ni rafiki kwa mtu ambaye njia nyingine za uzazi wa mpango zimemkataa
4. Uwezo wa mtu kubeba mimba unarudi ndani ya muda mfupi mara tu baada ya kutoa kitanzi au lupu, hivo kuwa rahisi kwa mtu kushika mimba kwa muda unaotaka bila usumbufu wowote,
Tofauti na matumizi ya njia zingine za uzazi wa mpango kama vile; sindano ambazo huweza kusababisha mwanamke kukaa kwa muda mrefu bila kushika mimba
MAUDHI MADOGO MADOGO YA NJIA HII YA KITANZI AU LUPU NI PAMOJA NA;
- Huhitaji utaalam mkubwa kidogo katika kukiweka,endapo kitakosewa kuwekwa huweza kuleta madhara mengine
- Kinatakiwa ukichunguze mara kwa mara hasa unapokwenda period au blid kama kipo au kimetoka na blid
- Huhitaji kuwekwa katika mazingira ya usafi sana ili mama asije kupata maambukizi mengine wakati wa uwekaji wake, kama vile maambukizi katika via vyake vya uzazi yaani PID.
•
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!