ORODHA YA MAGONJWA AMBAYO HUSUMBUA SANA WATOTO WADOGO(kuanzia mwaka 0-5)

 WATOTO

• • • • •

ORODHA YA MAGONJWA AMBAYO HUSUMBUA SANA WATOTO WADOGO(kuanzia mwaka 0-5)


Yapo magonjwa mbali mbali ambayo huwasumbua sana watoto wadogo kuanzia wanapozaliwa tu mpaka wanapofikisha umri wa miaka mitano(5). Na baadhi ya magonjwa haya ni chanzo kikubwa cha vifo kwa watoto wadogo. Namba hizi katika orodha hii hazimaanishi chochote,wala hakuna uhusiano wa namba hizi na uhatari wa ugonjwa, miongoni mwa magonjwa hayo ni pamoja na;


1. Ugonjwa wa homa ya manjano kwa watoto, ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Neonatal Jaundice, mtoto huweza kupatwa na tatizo hili ambalo huhusisha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha bilirubin kwenye damu ya mtoto. Na moja ya dalili kuu ya ugonjwa huu ni pamoja na mtoto kubadilika rangi ya ngozi pamoja na macho kuwa Manjano.


2. Mtoto mdogo kupatwa na tatizo la Colic, Shida hii huhusisha mtoto kulia sana ambapo wataalam wa afya huuita kama ugonjwa wa Colic endapo mtoto huyu hulia kwa zaidi ya masaa 3 kwa siku, zaidi ya siku 3 kwa wiki, na kwa zaidi ya wiki 3. Hakuna sababu ya moja kwa moja ya kutokea kwa tatizo hili japo baadhi ya wataalam wa afya wanasema huenda ikiwa ni gesi kujaa tumboni,vichocheo vya mwili kusabibisha tumbo kujivuta na kupata maumivu N.K


3. Ugonjwa wa kikohozi na kutapika, Tatizo hili kutokea hasa hasa pale mtoto anapopewa chakula au maziwa,ndipo huanza kukohoa sana na kutapika. Na kwa asilimia kubwa baada ya uchunguzi wa kina watoto hawa hugundulika na matatizo ya mapafu au kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.


4. Ugonjwa wa tumbo kuvimba au abdominal distention, ambapo mara nyingi watoto wenye shida hii hata kwenda choo pia inakuwa vigumu.


5. Ugonjwa wa mtoto kuishiwa na damu au kwa kitaalam tunaita Neonatal Anemia, ambapo kwa asilimia kubwa mtoto huzaliwa na matatizo katika Seli hai nyekundu za damu yaani Red blood cells,kitu ambacho husababisha seli hai hizi kufa kabla ya kukua na kusababisha upungufu wa damu mwilini.


6.Ugonjwa wa UTI kwa watoto wadogo, ambapo huambatana na tatizo la homa za mara kwa mara, watoto wadogo hupatwa sana na shida hii ya UTI ambapo moja ya kiashiria kikubwa kwamba mtoto ana maambukizi kwenye mfumo wake wa mkojo ni joto lake la mwili kupanda(Homa).


7. Magonjwa mbali mbali ambayo huhusisha mfumo mzima wa chakula pamoja na umeng'enyaji wake kwa mtoto, ambapo moja ya dalili kubwa ya magonjwa haya ni pamoja na mtoto kutapika na Kuharisha.


8. Magonjwa  mbali mbali ambayo huhusisha shida katika uumbaji wa mtoto mfano; tatizo la hydrocephalus, ambapo mtoto huzaliwa na kichwa kikubwa kuliko kawaida au tatizo la mgongo wazi kwa watoto ambapo hujulikana kama Spinal bifida.


9. Ugonjwa wa Utapiamlo ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Malnutrition, tatizo hili huwapata watoto wengi,ambapo linahusisha moja kwa moja swala la lishe duni kwa mtoto.


10. Ugonjwa wa hypoxic ischemic encephalopathy(HIE), ugonjwa ambao huhusisha ubongo kutokufanya kazi vizuri kutokana na ukosefu wa hewa ya oxygen ya kutosha kwenye ubongo. Ugonjwa huu husababisha vifo kwa watoto wengi.


11. Tatizo la mtoto kushikwa na Degedege, ambapo huhusisha dalili mbali mbali kama vile; mtoto kutingishwa na kutetemeshwa mwili.


12. Ugonjwa unaojulikana kama Cystic Fibrosis,ambapo ni tatizo la kurithi ambalo huhusisha viungo mbali mbali vya mtoto huathiriwa na kuharibiwa kama vile mapafu, N.K


13. Ugonjwa wa Moyo


14. Ugonjwa wa homa ya uti wa Mgongo(Meningitis), ambapo kwa asilimia kubwa hutokana na maambukizi ya Bacteria.


15. Ugonjwa wa pneumonia kwa watoto(Congenital Pneumonia) ambao huhusisha mtoto kupata shida sana ya upumuaji,Homa kali N.K


ANGALIZO; Mtoto anatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina baada ya kuzaliwa ikiwa ni pamoja na kuangalia vitu kama sehemu za siri za mtoto zipo sawa?,Korodani zimeshuka kama kawaida?,mtoto anakojoa? na kama anakojoa mkojo unapita kwenye tundu lake kama watu wengine au tundu la mkojo lipo sehemu nyingine?, mtoto anapata choo vizuri? au sehem ya haja kubwa imeziba?, N.K



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.







0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!