SAFARI YA UJAUZITO TOKA SIKU YA KWANZA UNAPATA MPAKA UNAJIFUNGUA

 MJAMZITO

• • • • • 

SAFARI YA UJAUZITO TOKA SIKU YA KWANZA UNAPATA MPAKA UNAJIFUNGUA


Safari hii ni ndefu kidogo na ina changamoto nyingi kutokana na mabadiliko mengi ambayo hutokea katika mwili wa Mwanamke. Lakini nikutoe hofu kwamba ukipata elimu ya kutosha hasa wewe ambaye ndyo mimba yako ya kwanza utaifurahia na kuikumbuka sana safari hii.


Kwa wastani au kawaida,safari hii huanza toka mama anavyopata mimba mpaka anapomaliza wiki 37 mpaka 40 au 42. Ikiwa pungufu ya hapo ni tatizo na ikiwa zaidi ya hapo pia kuna madhara yake.


Mabadiliko makubwa  ya vichocheo mwilini kipindi cha Ujauzito ndyo huleta mabadiliko makubwa ya mwili katika kipindi hiki,mambo mengi ya mwanamke hubadilika ikiwa ni pamoja na mtindo mzima wa maisha au lifestyle kama wengi walivyozoea kusema.


MABADILIKO AMBAYO HUTOKEA KIPINDI CHA UJAUZITO NI PAMOJA NA;


1. Mama mjamzito kutema mate sana


2. Mama mjamzito kukosa usingizi kabsa


3. Mama mjamzito kuanza kuwa na tumbo kubwa japo sio kwa wote pamoja na kuongezeka uzito wa mwili kadri mtoto anavyokuwa tumboni


4. Mama mjamzito kuanza kupenda baadhi ya vyakula na kuanza kuchukia baadhi ya vyakula Flani


5. Mama mjamzito kuanza kupenda harufu za vitu flani na kuanza kuchukia harufu za vitu flani, Mfano; Mama mjamzito huweza kuchukia harufu ya aina flani ya pafumu hivo akihisi tu hyo harufu huanza kupata kichefuchefu na kutapika


6. Mama mjamzito kuanza kupata kichefuchefu cha mara kwa mara pamoja na kutapika


7. Mama mjamzito kupatwa na tatizo la kiungulia au heartburn mara kwa mara


8. Mama mjamzito kupata choo gumu


9. Mama mjamzito kukojoa kojoa mara kwa mara


N.K


KUMBUKA; Moja ya vitu ambavyo mama mjamzito hutakiwa kuzingatia ni pamoja na kutokuvaa mavazi yanayombana tumbo au viatu virefu kwani huweza kuwa hatari kwake.


✓ Baada ya mama kuhisi tu ana mimba kwa protocol za afya hushauriwa mama huyo kwenda hosptal kwa ajili ya kupimwa na kama ni mjamzito,maandalizi mbali mbali yaanze kufanyika ikiwa ni pamoja na swala la kuanza kliniki.


Kumbuka; Kila hosptal huweza kuwa na utaratibu wake wa mda wa mama mjamzito kuanza kliniki ila protocol ya afya husema Mahudhurio ya kwanza ya Kliniki yaanze tu mama anapokuwa mjamzito na kabla ujauzito kufikisha wiki 16. Soma hapa chini kujua mahudhurio ya Kliniki kwa mama Mjamzito


MAHUDHURIO YA KLINIKI KWA MAMA MJAMZITO


1. Hudhurio la kwanza ni kabla ya ujauzito kifikisha wiki 16


2. Hudhurio la pili huanza ujauzito ukiwa na wiki 20 mpaka 24


3. Hudhurio la tatu huanza ujauzito ukiwa na wiki 28 mpaka 32


4. Hudhurio la nne huanza ujauzito ukiwa na wiki 36 mpaka 40


Japo mama mjamzito anaweza kuhudhuria mahudhurio zaidi ya manne kama kuna ulazima kulingana na hali yake ya ujauzito


Hayo ndyo baadhi ya mambo ambayo nimeyagusia katika safari ya Ujauzito ya Mwanamke ambapo nimezungumzia kuhusu baadhi ya mabadiliko ambayo hutokea kipindi cha ujauzito pamoja na mahudhurio ya kliniki kwa mama huyu.



KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!