SAMAKI
• • • • • •
SAMAKI NA AFYA YA MOYO,AKILI,UJAUZITO NA UZAZI
Ulishawah kuskia watu wakisema ukila vichwa vya samaki unakuwa na akili nyingi shuleni? Watu hawa hawapo mbali sana na ukweli,kwani sio vichwa tu bali samaki mzima ukimla husaidia afya ya akili yako. Katika makala ya Leo tunachambua umuhimu wa Samaki katika afya ya moyo,akili,ujauzito pamoja na Uzazi.
- Moja ya virutubisho muhimu sana kutoka kwa Samaki ni Virutubisho vingi aina ya Omega3 ambavyo hivi ndivyo husaidia kwa kiwango kikubwa kuukinga Moyo usishambuliwe na magonjwa mbali mbali.
- Uwepo wa Omega3 au Protein nyingi kwenye Samaki husaidia katika kujenga Ubongo wa Mtu wenye afya bora ikiwemo ni pamoja na afya ya akili.
- Ulaji wa samaki kwa wingi pia husaidia katika kujenga Mifupa yenye Nguvu na Mifupa Imara.
- Protein iliyopo ndani ya samaki husaidia katika kujenga misuli ya mwili
- Ulaji wa Samaki kwa Mama mjamzito,humsaidia sana katika uumbaji wa mtoto aliyetumboni,hasa hasa uumbaji unaohusisha ubongo,akili,uti wa mgongo pamoja na mfumo mzima wa fahamu kwa mtoto.
- Samaki wana kiwango kikubwa cha Madini ya Zinc ambayo ni muhimu sana katika kuimarisha Mfumo wa Uzazi, ndyo mana hata wanaume hushauriwa sana kutumia Samaki kwa wingi pia.
- Tafiti zinaonyesha kwamba ulaji wa samaki huleta uimara na afya ya Mbegu za mwanaume,na pia husaidia Nitric oxide katika kutanua mishipa ya damu ndani ya uume, hivo kwa namna moja au nyingine mbali na kuimarisha mbegu za kiume pia huweza kuimarisha nguvu za kiume.
Unashauriwa Ule Samaki angalau mara tatu au zaidi Ndani ya wiki moja,
KWA UJUMLA TUMEZUNGUMZIA UMUHIMU WA SAMAKI KATIKA MAENEO YAFUATAYO;
1. Kinga dhidi ya magonjwa ya moyo
2. Kuimarisha mifupa ya mwili
3. Kuleta afya ya Ubongo pamoja na akili
4. Kusaidia katika uumbaji wa mtoto kwa mama mjamzito ikiwemo kuboresha mfumo mzima wafahamu
5. Kusaidia katika kuboresha afya ya mbegu za kiume pamoja na kuimarisha nguvu za kiume.
6. Kusaidia katika kujenga misuli ya mwili
KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!