AFYA KWA WATOTO
• • • • • •
SOMA KUJUA UMUHIMU WA WATOTO KULALA MCHANA
Wazazi wengi huwalazimisha watoto kulala mchana bila kujua umuhimu wa kufanya hivo, wengine hawajui na wala hawafanyi jitihada za kuwalaza watoto mchana. Wengine hufanya hivo kupunguza vurugu na mikikimikiki ya watoto, Wengine wanafanya kwa sababu ya mazoea, kuiga kwa majirani na sababu nyingi zingine. Tambua umuhimu wa mtoto kulala mchana;
➡️ Husaidia ukuaji wa mtoto hasa wa ubongo na viungo vya mwili
➡️ Inaongeza ubunifu na ufanisi katika shule na maeneo mengine
➡️ Inaongeza uwezo wa kujifunza na kumbukumbu
➡️ Inapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo
Kwa sababu hizo ni muhimu sana wazazi kuhimiza watoto kulala mchana kwaajili ya afya bora na ukuaji bora.
Tunaweza kutoona faida yake mara moja lakini baadae tukaona matokeo makubwa hasa kwenye ukuaji wao na uwezo wa akili zao darasani, fikra zao na mambo yanayoendana na kuepuka magonjwa kama vile ya moyo. Mhimize mtoto alale mchana kwaajili ya afya bora.
Cc: @_afyazone
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!