BAMIA
• • • • • •
SOMA MAKALA HII KUJUA FAIDA ZA KULA BAMIA MWILINI(Chakula ni afya)
Bamia ni tunda linalotumiwa kama mboga kwa jamii nyingi za Tanzania.
Mara nyingi uchanganywa kwenye mboga mbalimbali kwa ajili ya kuongeza ladha ya mboga pia hutumika zenyewe kama mboga pia.
Inawezekana unakula bamia bila kujua zina faida gani mwilini kwako na zinasababisha nini mwilini mwako.
Pia yawezekana ukawa na tatizo la kiafya ambalo linahitaji kula bamia ili kutatua tatizo ulilonalo hivyo ni vizuri tukazijua faida za kula bamia.
Kabla ya kuangalia zina faida gani mwilini tuangalie kwanza bamia zina virutubisho gani ambavyo vinaingia mwilini.
Bamia ina wingi wa Vitamini A, B, C, E na Vitamini K.
Vilevile bamia zina wingi wa madini chumvi ya Kalshiamu, chuma, Magneshiamu, Potashiamu pamoja na zinki.
FAIDA ZA KULA BAMIA MWILINI(Chakula ni afya)
Zifuatazo ni faida za kula bamia:-
1. KUIMARISHA MFUMO WA UMENG'ENYAJI CHAKULA.
Bamia zinasaidia kuimarisha mfumo wa umeng’enyaji chakula.
Kutokana na bamia kuwa na wingi wa nyuzi lishe husadia kuimarisha utendaji kazi wa mfumo chakula kwa kukifanya chakula kipite vizuri na kumeng’enywa vizuri hivyo kukupunguzia matatizo mbalimbali ya tumbo kama vile tumbo kujaa gesi pamoja na mgandamano wa chakula kwenye utumbo. Pia bamia zinaweza kuzuia kuharisha.
2. KUIMARISHA UWEZO WA KUONA.
Bamia ina wingi wa Vitamini A.
Vitamin A imekuwa msaada mkubwa sana kwa matatizo mbalimbali ya macho.
Si tu vitamin A inayopatikana kwenye bamia pia kuna virutubisho vingine ambacyo huondoa sumu mbalimbali mwilini hasa zile ambazo zinazoweza kusababisha kufa kwa seli za macho. Hivyo basi matumizi ya bamia mara kwa mara inakupunguzia uwezekano wa kupata upofu.
3. BAMIA NI MSAADA KWA AFYA YA NGOZI.
Mbali na kuwa msaada kwa macho pia vitamin A kwenye bamia ina msaada kwa afya ngozi.
Hivyo matumizi ya bamia kunaifanya ngozi kama ina jeraha kupona haraka na kupunguza chunusi na makovu mwilini.
Vilevile huondoa makunyanzi kwenye ngozi.
4. KUIMARISHA KINGA YA MWILI DHIDI YA MAGONJWA MBALIMBALI.
Kutokana na uwepo wa virutubisho mbalimbali ambavyo huondoa sumu mbalimbali mwilini pamoja na vitamin C kwenye bamia imekuwa ni msaada katika kinga ya mwili.
Cc:@_afyazone
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!