TAMBUA UGONJWA WA KUSHINDWA KUTAMBUA HARUFU(au kwa kitaalam anosmia)

ANOSMIA

• • • • • •

TAMBUA UGONJWA WA KUSHINDWA KUTAMBUA HARUFU(au kwa kitaalam anosmia)


NINI HUTOKEA?


Uwezo wa kunusa na kutambua harufu huongozwa na mfumo ufuatao; Baada ya 'molecule' kutoka katika unachonusa na kuamsha seli za neva ziitwazo 'olfactory'. Seli hizi hutuma taarifa kwenda katika ubongo na kutambua harufu husika. CHOCHOTE kitakacho ingiliana na mfumo huu hupelekea kukosa uwezo wa kutambua harufu, aidha kwa muda ama wa kudumu. .

.

Uwezo wa kunusa pia huathiri utambuzi wa ladha ya chakula. Kukosekana kwa uwezo huu, hupelekea seli za 'taste buds' kushindwa kutambua ladha za vitu mbalimbali. 


Bila ya uwezo wa kunusa, chakula huwa na ladha tofauti, huwezi kutambua harufu ya maua na vitu vingine na unaweza kupata madhara kama; unaposhindwa kunusa na kutambua harufu utashindwa kunusa gesi inayovuja katika mtungi na kuweza kuleta madhara makubwa. .

.

VISABABISHI 


1. Kuziba kwa pua kutokana na mafua, mzio/aleji, maambukizi ya sinus au uvutaji wa hewa chafu 


2. Vinyama vya puani


3. Jeraha katika pua na seli za neva kutokana na upasuaji au ajali ya kichwa 


4. Kuvuta hewa ya kemikali-sumu kama dawa za wadudu mashambani n.k


5. Kutumia madawa ya kulevya ya Cocaine 


6. Uzee, kama ilivyo kwa uoni na usikivu, Uwezo wa kunusa pia hupungua kadri umri unavyosogea


7. Baadhi ya maradhi kama ya Alzheimer


8. Matibabu ya mionzi kwa saratani zinazohusisha kichwa au shingo


9. Uvutaji sigara


MATIBABU 


Kama tatizo limesababishwa na kuziba kwa pua, vinyama vya pua, majeraha basi ni kumuona daktari na kutibu tatizo husika. Pia, epuka uvutaji sigara. .

.

Kuhusiana na umri mkubwa (uzee), anosmia haitibiki bali unaweza kuepuka madhara, kwa mfano; Weka alarm za moto au moshi (fire detectors/smoke alarms) nyumbani ama ofisini. Pia, kama una mashaka na harufu ya kuoza kwa chakula ni vyema usikile. 

Cc; drtareeq




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!