CHANGO LA UZAZI
• • • • • •
TATIZO LA CHANGO LA UZAZI KWA WANAWAKE,CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE
Tatizo hili halitokei kwa Wanawake tu, kuna chango la Uzazi kwa Wanaume pia(Watu wengi hawajui hili),
ila katika makala hii tunazungumzia kuhusu chango la Uzazi kwa Wanawake ikiwemo ni pamoja na chanzo chake,Dalili zake pamoja na matibabu yake.
CHANZO CHA TATIZO HILI LA CHANGO LA UZAZI KWA WANAWAKE NI PAMOJA NA;
1. Mwanamke kuwa na uzito mkubwa au uzito uliopitiliza huweza kupata tatizo hili la chango la uzazi
2. Mwanamke kukumbwa na hali ya kuzalisha vichocheo aina ya Prolactin kwa wingi sana kwenye damu,
hivo kupelekea kuathiri uzalishwaji wa vichocheo aina ya Estrogen ambavyo husaidia katika uzalishaji/upevushaji wa mayai kwenye vifuko vya mayai
3. Mwanamke kupatwa na Tatizo la kuziba mirija yake ya uzazi huweza kusababisha kupata tatizo hili la chango la Uzazi
4. Mwanamke kupatwa na maambukizi mbali mbali ya Magonjwa,
ikiwemo pamoja na maambukizi katika via vyake vya uzazi au kwa kitaalam tunaita pelvic inflammatory disease(PID)
5. Mwanamke kupatwa na tatizo la vifuko vya mayai kushindwa kufanya uzalishaji wa mayai pamoja na ukuaji wake kwa mda unaotakiwa
6. Mwanamke kupatwa na shida ya Mvurugiko wa vichocheo vya mwili ambao huchangiwa na sababu mbali mbali kama! matumizi ya baadhi ya Njia za uzazi wa mpango N.K
7. Pia matumizi ya tumbaku huweza kuchangia uwepo wa tatizo hili la chango la uzazi kwa Wanawake
DALILI ZA CHANGO LA UZAZI KWA WANAWAKE NI PAMOJA NA;
- Mwanamke kupatwa na maumivu makali wakati wa tendo la Ndoa
- Mwanamke kupata maumivu makali ya tumbo mara kwa mara
- Mwanamke kupata maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi
- Joto la mwili kupanda au Mwanamke kuwa na homa kila anapoingia siku zake
- Mwanamke kuwa na hasira za mara kwa mara hasa wakati wa hedhi
- Siku za kwenda hedhi kubadilika kabsa na kutokuwa na mpangilio maalum
N.K
WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA CHANGO LA UZAZI
1. Wanawake zaidi ya Wanaume
2. Wenye uzito mkubwa au Wanene
3. Wenye maambukizi ya Magonjwa katika via vya Uzazi
4. Wanywa Pombe au Walevi
5. Watumiaji wa sigara ikiwa ni pamoja na tumbaku
N.K
MATIBABU YA CHANGO LA UZAZI KWA WANAWAKE
Hakuna tiba ya moja kwa moja kwa ajili ya chango la Uzazi,
japokuwa Kuna tiba ya kidhibiti dalili ambazo mgonjwa wa chango la uzazi huzipata hii ikiwa ni pamoja na kupata Dawa za kutuliza maumivu ya tumbo,
dawa za kurekebisha mabadiliko ya vichocheo mwilini, Dawa za kushusha homa kwa Mgonjwa N.K
KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!