NYWELE KUKATIKA
• • • •
TATIZO LA KUKATIKA KWA NYWELE(chanzo chake na tiba yake)
Tatizo hili la nywele kukatika kwa asilimia kubwa wamekuwa wakilalamika wanawake kwani ndyo huhusika zaidi na mambo ya urembo wa nywele bila kujua kwamba hata wanaume pia hupatwa na tatizo hili la nywele kukatika.
katika hali ya kawaida mtu akichana nywele kwa kutumia chanuo, nywele hizo huweza kukatika, lakini hali hii huweza kuwa tatizo pale ambapo mtu hukatika nywele nyingi kwa wakati mmoja.
SABABU AU CHANZO CHA NYWELE KUKATIKA NI NINI?
- Nywele huweza kukatika kutokana na upungufu wa virutubisho aina ya protein kwenye mwili wako, kwani protein ndyo huleta afya ya nywele ikiwa ni pamoja na ukuaji wake
- Kuwa na magonjwa ya kisaikolojia ikiwa ni pamoja na yale ambayo husababisha hali kubwa ya msongo wa mawazo, pia huweza kuleta shida hii ya nywele kukatika
- Uvutaji wa sigara huweza kusababisha pia tatizo hili la nywele kukatika
- Tatizo la mvurugiko wa vichocheo mwilini yaani kwa kitaalam hormone imbalance
- Kuwa na magonjwa yanayohusu mfumo mzima wa damu kichwani
- Kwa mama mjamzito na mama baada ya kujifungua. Tatizo hili hutokea sana kwa wakina mama wengi wajawazito na wengine baada tu ya kujifungua na hii ni kutokana na kwamba kwa asilimia kubwa, virutubisho vinavyohusika na kuleta afya mwilini ikiwa ni pamoja na afya ya nywele hutumiwa na mtoto aliyetumboni na anayenyonya.
Lakini pia hali ya kuwa mjamzito husababisha kinga ya mwili kwa mama mjamzito kuwa chini au kushuka hali ambayo huweza kupelekea shida hii pia.
- Tatizo la kurithi vinasaba vya tatizo hili katika koo au familia husika. Hivo tatizo hili la nywele kukatika huweza kuwa la kurithi pia
- Kupatwa na magonjwa mbali mbali ambayo husababisha kinga ya mwili kushuka kama vile ukimwi
- Matumizi ya baadhi ya dawa za nywele ambazo zina makemikali hatari kwa afya ya nywele pamoja na ngozi. Mfano dawa za nywele zenye kemikali aina ya hydrogen perioxide sio salama kwa afya ya nywele na ngozi yake.
MATIBABU YA TATIZO LA NYWELE KUKATIKA
• Matibabu ya tatizo hili hutegemea na chanzo husika,kama nilivyokwisha kuelezea vyanzo mbali mbali hapo juu.
Hivo ni muhimu kwenda hospital au kuongea na wataalam wa afya kwanza ilikujua chanzo cha shida yako. Ndipo matibabu yaanzie hapo
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
muhimu
new
post
uzazi
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!