TATIZO LA KWENYE NGOZI AMBALO HUJULIKANA KAMA DERMATOSIS PAPULOSA NIGRA(Chanzo chake,Dalili Pamoja na Matibabu yake)

 DERMATOSIS PAPULOSA NIGRA

• • • • •

TATIZO LA KWENYE NGOZI AMBALO HUJULIKANA KAMA DERMATOSIS PAPULOSA NIGRA(Chanzo chake,Dalili Pamoja na Matibabu yake)



Tatizo hili huhusisha mtu kuwa na vidoti vyeusi kwenye ngozi maarufu kama vishangazi ambavyo hupendelea kutokea maeno ya usoni pamoja na shingoni.


CHANZO CHA TATIZO HILI LA DERMATOSIS PAPULOSA NIGRA


Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo husababisha mtu kupatwa na tatizo hili, japo tafiti zinaonyesha kuna baadhi ya vitu ambavyo huongeza uwezekano wa mtu kupatwa na tatizo hili la kwenye ngozi na vitu hivo ni pamoja na;


- Kuwa na mtu ambaye katika ukoo wenu ana vidoti hivi, ambapo tafiti huonyesha huenda vinasaba vinaweza kurithiwa katika tatizo hili la vidoti kwenye ngozi.


- Kuwa na ngozi nyeusi, tafiti zinaonyesha kwamba wanaopatwa na vidoti hivi ni watu wenye ngozi nyeusi zaidi kuliko wengine, hivo huenda kuwa na ngozi nyeusi sana ikachangia mtu kupatwa na tatizo hili la vidoti kwenye Ngozi.


MATIBABU YA TATIZO LA DERMATOSIS PAPULOSA NIGRA


Vidoti hivi havina madhara yoyote kwenye ngozi ya mtu na wala havihitaji tiba yoyote. Hivo ni hali ya kawaida tu wala hakuna tatizo.


Ingawa kama unapata sana miwasho katika maeneo ya vidoti hivi nenda hosptal ukaongee na wataalam wa afya hasa wataalam wa magonjwa ya Ngozi watakusaidia.


KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!