TATIZO LA UKE KUTOA MAJI MAJI(Ambayo huwa na harufu mbaya)

 AFYA YA UKE

• • • • •

TATIZO LA UKE KUTOA MAJI MAJI(Ambayo huwa na harufu mbaya)


Shida hii huwapata wanawake wengi kwa hivi sasa, Lakini pia kwa baadhi ya wanawake maji haya hayana harufu mbaya ila hutoka mara kwa mara na kuchafua nguo za ndani na wengine maji haya huambatana na harufu mbaya.


CHANZO CHA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


• Maambukizi ya magonjwa mbali mbali Mfano; maambukizi katika via vya Uzazi vya mwanamke PID, ikiwemo pamoja na maambukizi kwenye Mlango wake wa uzazi(Cervix) au maambukizi ya bacteria kwenye damu.  Hapa kwa asilimia kubwa wanawake hawa hutokwa na maji maji ukeni mara kwa mara ambayo huambatana na harufu mbaya.


• Mabadiliko ya vichocheo mwilini ambayo husababisha tezi linalohusika na kuleta hali ya ute ute pamoja na maji maji ukeni,kuzidi kuzalisha maji zaidi ya kiwango cha kawaida, hivo kupelekea mwanamke kutokwa na maji maji mara kwa mara.Japo mara nyingi maji haya hayana harufu mbaya.


MATIBABU YA TATIZO HILI


Matibabu ya tatizo hili hutegemea chanzo chake; kama chanzo ni maambukizi katika via vya uzazi au PID, basi mwanamke huyu atapewa dawa za PID kama vile doxcycline N.K 


Na kama chanzo cha tatizo hili ni mvurugiko wa vichocheo mwilini, basi mwanamke atapewa dawa za kurekebisha vichocheo mwilini au Hormones.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!