MARBURG
• • • • •
UFAHAMU UGONJWA WA HOMA YA KUVUJA DAMU AU UGONJWA WA MARBURG
Huu ni ugonjwa ambao unafananishwa na Ebola kwa dalili zake, ila ugonjwa huu wa homa ya kuvuja damu ni ugonjwa ambao unasababishwa na Virusi ambavyo vinajulikana kwa kitaalam kama MARBURG.
Licha ya kuathiri binadamu,ugonjwa huu wa homa ya kuvuja damu huweza Pia kushambulia wanyama mbali mbali kama vile; wanyama jamii ya Sokwe,Nyani N.K
DALILI ZA UGONJWA WA HOMA YA KUVUJA DAMU(MARBURG) NI PAMOJA NA;
1. Mgonjwa kuanza kuvuja damu maeneo mbali mbali ya mwili yenye uwazi mfano; Mdomoni,Puani na masikioni
2. Mgonjwa kuanza kujisaidia haja kubwa ya maji mengi (kuharisha maji mengi)
3. Mgonjwa kupatwa na hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika
4. Joto la mwili la Mgonjwa kupanda au Mgonjwa kuwa na homa
5. Mgonjwa kupata uchovu sana katika mwili wake pamoja na mwili kukosa nguvu
6. Mgonjwa kupata maumivu makali kwenye misuli ya mwili,joint pamoja na viungo mbali mbali vya mwili
7. Mgonjwa kukosa hamu ya chakula
8. Mgonjwa kupata maumivu makali ya tumbo
9. Mgonjwa kuhisi hali ya vichomi
10. Mgonjwa kupata maumivu makali ya kichwa mara kwa mara
MATIBABU YA UGONJWA WA HOMA YA KUVUJA DAMU(MARBURG)
Hakuna tiba wala chanjo kwa ajili ya kutibu na kuzuia Ugonjwa huu wa homa ya kuvuja damu au ugonjwa wa marburg, Hivo kama ilivyo magonjwa mengi yanayosababishwa na Virusi,Mgonjwa hutibiwa dalili za ugonjwa huu wa kuvuja damu, Mfano; Kama Mgonjwa anapata maumivu makali ya misuli,joint pamoja na viungo vya mwili basi hupewa dawa za kudhibiti maumivu hayo N.K
•
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA KUHUSU TATIZO LOLOTE LA KIAFYA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!