CHEMBE YA MOYO
• • • •
UGONJWA WA CHEMBE YA MOYO(chanzo,dalili na tiba yake)
Ugonjwa wa chembe ya moyo au kwa kitaalam huitwa angina pectoris ni ugonjwa wa moyo ambao huhusisha maumivu makali ya upande wa kushoto mwa kifua na wakati mwingine maumivu haya husambaa hadi mashavuni,shingoni, mgongoni,mkono wa kushoto N.K
CHANZO CHA UGONJWA HUU WA CHEMBE YA MOYO
Chanzo kikubwa cha ugonjwa huu wa moyo wa chembe ya moyo(angina pectoris), ni kutokana na shida kwenye mishipa ya damu ya moyo hali ambayo hupelekea kuwepo kwa kiwango kidogo cha damu kwenye mishipa ndani ya moyo pamoja na ukosefu wa hewa ya oxygen ya kutosha
Tatizo hili la kwenye mishipa ya moyo huchangiwa na baadhi ya vitu mbali mbali kama vile;
• Ulaji wa vyakula vyenye mafuta kwa kiasi kikubwa sana
• Ulali wa vyakula jamii ya wanga kwa wingi sana
• Matumizi ya pombe kupita kiasi
• Uvutaji wa sigara
• Kupatwa na tatizo la presha
• Uzito kupita kiasi pamoja na unene wa mwili
• Kuwa na tatizo la msongo wa mawazo mara kwa mara
• Kupatwa na hali ya hofu kuu kila mara
• Kuwa na ugonjwa wa kisukari
N.K
DALILI ZA UGONJWA HUU WA CHEMBE YA MOYO NI PAMOJA NA;
- Mgonjwa kupata maumivu makali ya upande wa kushoto mwa kifua na wakati mwingine maumivu haya husambaa hadi mashavuni,shingoni, mgongoni,mkono wa kushoto N.K
- Hali ya kushindwa kupumua au kupata shida ya upumuaji
MATIBABU YA UGONJWA HUU WA CHEMBE YA MOYO
Endapo umepata dalili kama hizi ni vizuri kwenda hosptal kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili upate matibabu
VITU VYA KUEPUKA
✓ Epuka ulaji wa vyakula vya mafuta sana
✓ Epuka uvutaji wa sigara
✓ Epuka matumizi ya pombe kupita kiasi
✓ Epuka kula vyakula vya wanga kwa kiasi kikubwa
✓ Fanya mazoezi ya mwili wako
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!