BERIBERI
• • • •
UGONJWA WA BERIBERI(chanzo,dalili na tiba)
Ugonjwa wa beriberi ni ugonjwa ambao chanzo chake kikubwa ni upungufu na ukosefu wa vitamins aina ya vitamin B1 au Thiamine.
DALILI ZA UGONJWA WA BERIBERI NI PAMOJA NA;
1. Kupatwa na shida ya ngozi kuwa na madoa doa hasa kwenye viganja vya mikono
2. Kupatwa na tatizo la kuwashwa kwenye ngozi
3. Kupatwa na shida ya mtu kupepesa macho au macho kucheza cheza bila kujizuia
4. Kupatwa na tatizo la kuvimba miguu
5. Kupata shida wakati wa kuvuta na kutoa hewa
6. Kupatwa na tatizo la miguu kukosa nguvu pamoja na kupooza
7. Wengine kushindwa kutembea kabsa
8. Shida ya mapigo ya moyo kubadilika
9. Wakati mwingine ngozi ya mwili kukakamaa
N.K
MATIBABU YA UGONJWA WA BERIBERI
- Matibabu ya ugonjwa wa beriberi yote ni kuongeza vitamins aina ya Vitamin B1 au thiamine, Hivo njia mbali mbali hutumika kama;
• Mgonjwa wa beriberi kupewa virutubisho vya thiamine au Vitamin B1 kwa njia ya vidonge au Sindano
• Lakini pia kula vyakula ambavyo vinaongeza vitamin B1 au thiamine kwa wingi sana
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!