UGONJWA WA CANDIDIASIS(maana,chanzo,dalili na tiba yake)

 FANGASI

• • • • •

UGONJWA WA CANDIDIASIS(maana,chanzo,dalili na tiba yake)


Ugonjwa wa candidiasis, huu ni ugonjwa ambao huhusisha mashambulizi ya Fangasi katika maeneo tofauti ya mwili wa binadamu Kama vile; Sehemu za siri ambapo kwa kiasi kikubwa hushambuliwa na Fangasi wanaojulikana kwa jina la Candida Albicans.


Mashambulizi haya ya Fangasi(Fungal Infection) huweza kuhusisha maeneo mbali mbali ya mwili wa binadamu kama vile;


- Damu


- Sehemu za siri


- Kooni


- Miguuni


- Mikononi


- Kwenye ngozi


- Mdomoni


- Kwenye Ulimi

N.K


DALILI ZA UGONJWA WA CANDIDIASIS( hasa katika sehemu za Siri)


- Miwasho sehemu za siri ikiwa ni pamoja na eneo lote la ngozi ya korodani mpaka katikati ya njia ya haja kubwa na uume, Kwenye mashavu ya uke na eneo lote kuzunguka hapo.


- Kupatwa na vidonda pamoja na michubuko sehemu za siri


- Ngozi ya sehemu za siri kubadilika rangi na kuwa nyekundu


- Kutokwa na uchafu wenye rangi na mzito kama maziwa mgando


- Maumivu ya tumbo chini ya kitovu


- Kupatwa na vipele vidogo vidogo sehemu za siri

N.K


 MATIBABU YA UGONJWA WA CANDIDIASIS


- Matibabu ya ugonjwa wa candidiasis huhusisha matumizi ya dawa mbali mbali kama vile; Clotrimazole cream ya kupaka pamoja na tube za kudumbukiza ukeni, Fluconazole, Griseofulvin, N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!