DEGEDEGE
• • • • • •
UGONJWA WA DEGEDEGE(chanzo,dalili na tiba yake)
Hili ni tatizo ambalo linahusisha hali ya mwili pamoja na viungo kama mikono na miguu kutingishwa au kutetemeshwa, tatizo hili huleta hali ya kukakamaa kwa misuli ya mwili wa binadamu.
Tatizo la degedege huweza kumpata mtu wa umri wowote ule,japo kuna makundi ya watu ambao wapo kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la Dege dege.
MAKUNDI AMBAYO YAPO KWENYE HATARI YA KUPATA TATIZO LA DEGEDEGE NI PAMOJA NA;
- Watoto wadogo
- Mama wajawazito
- Wenye magonjwa yanayosababisha mwili kushindwa kudhibiti kiwango cha sukari kwenye Damu
- Wenye matatizo la kuishiwa na pumzi,kushindwa kupumua na kukosa hewa ya Oxygen
- Ambao wapo kwenye familia ambazo kuna watu wanaopata tatizo hili
- Mwanamke ambaye aliwahi kupata tatizo la degedege kwenye ujauzito uliopita
- Mtu ambaye alishawah kupata tatizo la degedege angalau mara moja kwenye maisha yake
- Vijana
CHANZO CHA TATIZO LA DEGEDEGE
Tatizo la degedege kwa asilimia kubwa husababishwa na ubongo wa mtu kushambuliwa na baadhi ya magonjwa au kuwa na tatizo la kushindwa kufanya kazi vizuri ambapo hupelekea upungufu wa vichocheo vya Sukari kwenye damu yaani kwa kitaalam Hypoglycemia pamoja na kuwa na upungufu wa hewa ya oxygen kwenye Damu yaani kwa kitaalam hypoxia.
Hata hivo tatizo la dege dege huweza kuhusishwa na magonjwa yanayoshambulia Uti wa Mgongo kama Vile homa ya Uti wa mgongo pamoja na Magonjwa mengine kama MALARIA.
DALILI ZA TATIZO LA DEGEDEGE NI PAMOJA NA;
• Misuli ya mwili pamoja na viungo kama mikono na miguu kukakamaa
• Hali ya kupinda shingo na kurudisha kichwa nyuma
• Hali la mwili kutetemeka au kutingishwa
• Hali ya kutoa mapovu Mdomoni
• Kupata shida ya upumuaji
• Kupatwa na shida ya macho kugeukia kwa nyuma na kuonekana weupe wa jicho tu huku weusi wa jicho ukipotea
• Kushindwa kudhibiti utokaji wa mkojo pamoja na haja kubwa
• Kuwa na shida ya kupoteza kumbukumbu
• Mgonjwa kupoteza Fahamu kabsa
MATIBABU YA TATIZO LA DEGEDEGE
Matibabu ya tatizo la degedege hutegemea chanzo cha tatizo hili, Mfano; endapo tatizo la degedege limesababishwa na magonjwa ya Uti wa mgongo kama homa ya uti wa mgongo au magonjwa mengine kama Malaria,vivyo hivyo matibabu yatakuwa ni ya kutibu Malaria pamoja na homa ya Uti wa mgongo.
Endapo Mgonjwa ana dalili zozote za Degedege ni vizuri kuwahishwa hospital haraka kwa ajili ya vipimo na kuanza matibabu kamili.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!