DENGUE
• • • • •
UGONJWA WA DENGUE(chanzo,dalili na tiba yake)
Ugonjwa wa Dengue ni ugonjwa ambao chanzo chake ni virusi ,ugonjwa huu huweza kusambazwa na mbu ambao wamebeba vimelea hivi.
CHANZO CHA UGONJWA WA DENGUE
Hivo basi kama nilivyokwisha kusema hapo juu ugonjwa wa dengue chanzo chake ni virusi lakini msambazaji mkuu ni mbu jamii ya Aedes aegypti na wakati mwingine hata jamii ya Aedes albopictus huhusika pia.
DALILI ZA UGONJWA WA DENGUE NI PAMOJA NA;
- Joto la mwili la mgonjwa kupanda au mgonjwa kuwa na homa
- Kupata uchovu wa mwili kupita kiasi
- Kupata maumivu makali ya kichwa
- Mgonjwa kukosa kabsa hamu ya chakula
- Maumivu ya viungo,misuli pamoja na joint kwenye mwili
- Maumivu ya tumbo,kiuno na mgongo
Maeneo ya joto sana, pamoja na hali ya unyevu unyevu huweza kuwa mazingira mazuri sana ya ugonjwa huu
MATIBABU YA UGONJWA WA DENGUE
Homa ya dengue huweza kutibika kwa njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa aina mbali mbali,
Ushauri wangu kwako ni bora kwenda hospital kufanya vipimo kwanza, kabla ya kuanza matibabu
@Kwa Ushauri zaidi,Elimu, Au Tiba tuwasiliane kwa Namba +255758286584
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!