Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA KUDHOOFIKA KWA MISULI YA MWILI(MUSCULAR DYSTROPHY)



KUDHOOFIKA MISULI

• • • • • •

UGONJWA WA KUDHOOFIKA KWA MISULI YA MWILI(MUSCULAR DYSTROPHY)


Ugonjwa huu wa kudhoofika kwa misuli ya mwili ambao kwa kitaalam hujulikana kama Muscular Dystrophy huweza kusababisha hali ya ulemavu wa viungo kwa Mtu, na tafiti zinaonyesha kwamba shida hii hutokea katika vinasabab vya mtu,hivo huweza kurithiwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine katika ukoo flani.


Tafiti zinaonyesha kwamba watu ambao wapo kwenye familia ambazo kuna mtu mwenye shida hii,wapo kwenye hatari pia ya kupatwa na shida hii, lakini pia tatizo hili la kudhoofika kwa misuli ya mwili yaani kwa kitaalam Muscular Dystrophy huathiri jinsia ya kiume zaidi ya ile ya kike kwa asilimia kubwa.


CHANZO CHA TATIZO HILI LA KUDHOOFIKA KWA MISULI YA MWILI


- Tatizo hili la mtu kudhoofika misuli yake ya mwili hutokea pale ambapo kuna shida katika mgawanyiko pamoja na muingiliano wa vinasaba ambavyo hutengeneza protini kwa ajili ya kuunda na kutengeneza misuli imara ya mwilini,hivo shida hii kupelekea madhara mbali mbali mwilini ikiwemo hili la misuli ya mwili kudhoofika.


DALILI ZA TATIZO HILI LA KUDHOOFIKA KWA MISULI YA MWILI NI PAMOJA NA;


1. Misuli ya mwili kutokuwa na nguvu au kuwa dhaifu


2. Tatizo la Mgonjwa kushindwa kusimama au hata kukaa wakati amelala


3. Mgonjwa kupatwa na shida ya kudondoka hali ambayo hujirudia rudia


4. Mgonjwa kushindwa kutembea mwenyewe bila msaada wa kitu chochote au kutembea kwa kupinda pinda


5. Mgonjwa kupatwa na maumivu makali ya misuli pamoja na misuli ya mwili kukakamaa


6. Tatizo la mgonjwa kuwa na viungo vya mwili ambavyo havipo kawaida mfano; mgonjwa kuwa na shingo Ndefu,Sura ndefu N.K


MATIBABU YA TATIZO HILI LA MTU KUDHOOFIKA KWA MISULI YAKE YA MWILI



Hakuna tiba au dawa za moja kwa moja kwa ajili ya kutibu na kudhibiti tatizo hili, hivo mgonjwa hupata matibabu ya dalili tu za ugonjwa huu lakini sio kutibu kabsa chanzo cha tatizo hili.



KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.







Post a Comment

0 Comments