LEISHMANIASIS
• • • • • •
UGONJWA WA LEISHMANIASIS,CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE
Huu ni ugonjwa ambao huhusisha kutokea kwa vidonda katika sehemu mbali mbali za ngozi ya mwilini au kwa kitaalam tunasema ni Ulcerative disease, Mfano tazama kwenye picha ya makala hii utaona mtu mwenye kidonda mkononi ambacho kimesababishwa na ugonjwa huu wa Leishmaniasis.
Ugonjwa huu wa Leishmaniasis kwa hapa Tanzania umeenea sana maeneo ya Kigoma,Tabora pamoja na Morogoro.
CHANZO CHA UGONJWA HUU WA LEISHMANIASIS
Ugonjwa huu wa Leishmaniasis ni ugonjwa ambao husababishwa na vimelea vya Protozoa jamii ya Leishmania na kusambazwa na nzi wa Mchangani yaani kwa kitaalam Sandflies. Hivo basi binadamu hupata maambukizi ya Leishmania kwa kung'atwa na hawa nzi wa mchangani.
DALILI ZA UGONJWA WA LEISHMANIASIS NI PAMOJA NA;
- Mgonjwa kupata vidonda kwenye maeneo tofauti ya Ngozi ya mwili ikiwa ni pamoja na sehemu ambapo ameng'atwa na hawa nzi wa mchangani(sandflies)
- Joto la mwili kwa mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa
- Mgonjwa kupatwa na shida ya kuvimba viungo mbali mbali ndani ya mwili ikiwa ni pamoja na ini kuvimba
- Kiwango cha seli hai nyekundu za damu(red blood cells) kwa Mgonjwa kushuka na kupelekea matokeo mbali mbali kama upungufu wa damu mwilini N.K,hii pia ni mojawapo ya dalili ya ugonjwa huu wa Leishmaniasis
MATIBABU YA UGONJWA HUU WA LEISHMANIASIS
Kulingana na dalili za Ugonjwa huu wa Leishmaniasis,zipo tiba mbali mbali ambazo mgonjwa wa tatizo hili huweza kupata,na baadhi ya tiba hizo ni matumizi ya dawa mbali mbali kama vile; Dawa ya Amphotericin B, Pentamidine, Fluconazole N.K
•
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!