UGONJWA WA TETEKUWANGA, CHANZO,NJIA ZA KUPATA,DALILI PAMOJA NA MATIBABU YAKE
TETEKUWANGA
• • • • •
UGONJWA WA TETEKUWANGA, CHANZO,NJIA ZA KUPATA,DALILI PAMOJA NA MATIBABU YAKE
Ugonjwa huu wa tetekuwanga au wengine huita matetekuwanga, hupendelea kutokea kwa watoto zaidi ya watu wazima, japo pia mtu mzima anaweza kupata,ingawa endapo utapata ugonjwa wa matetekuwanga katika umri mkubwa dalili zake huwa mbaya zaidi,na wengine hata kupoteza maisha kabsa.
Japo bahati nzuri ni kwamba, ukiumwa mara moja huwezi kuumwa tena na ugonjwa huu wa tetekuwanga kwani kinga ya mwili hutengeza memory cells kwa ajili ya ugonjwa huu, hivo mwili unakuwa na kinga ya kutosha na kutoshambuliwa na ugonjwa huu tena kwa mara nyingine.
CHANZO CHA UGONJWA WA TETEKUWANGA
- Ugonjwa wa tetekuwanga husababishwa na virusi aina ya Varicella Zoster na pia virusi hawa huweza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, hivo kuwa karibu na mtu mwenye ugonjwa wa tetekuwanga huweza kukusababisha na wewe kuumwa tetekuwanga.
NJIA AMBAZO MTU HUWEZA KUPATA UGONJWA WA TETEKUWANGA
✓ Mtu huweza kupata ugonjwa wa tetekuwanga kwa kupitia kugusa majimaji yanayotoka kwenye vipele vya mgonjwa
✓ Lakini pia unaweza kupata ugonjwa wa tetekuwanga kwa kupitia jasho la Mgonjwa wa tetekuwanga,mate,makohozi au wakati wa kupiga Chafya.
DALILI ZA UGONJWA WA TETEKUWANGA NI PAMOJA NA;
1. Kuwa na vipele vye maji maji katika maeneo mbali mbali ya mwili ikiwa ni pamoja na usoni
2. Kupatwa na miwasho mikali kwenye maeneo yote ya vipiele hivo kupelekea hali ya mgonjwa kujikuna sana
3. Joto la mwili la mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kupandisha homa
4. Mgonjwa wa tetekuwanga hupatwa na maumivu makali ya kichwa mara kwa mara
5. Mgonjwa kupoteza kabsa hamu ya chakula
6. Mgonjwa kupatwa na maumivu kwenye maeneo yote yenye upele hasa baada ya kujikuna na vipele kupasuka na kuanza kutoa majimaji
MATIBABU YA UGONJWA WA TETEKUWANGA
Hakuna matibabu ya moja kwa moja ya kutibu ugonjwa wa tetekuwanga unaosababishwa na Virusi vya Varicella Zoster.Hivo basi kama ilivyo matibabu ya magonjwa mengi yanayosababishwa na virusi,mgonjwa wa tetekuwanga hupewa dawa za kutibu na kudhibiti dalili za tete kuwanga, Mfano dawa za maumivu, dawa za kushusha joto la mwili au homa,dawa za kichwa Kuuma,dawa za kuzuia hali ya miwasho,N.K
•
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!