UKISIKIA TATIZO LA UMEME WA MOYO(ATRIAL FIBRILLATION) UNAELEWA NINI?

MOYO

• • • • • •

UKISIKIA TATIZO LA  UMEME WA MOYO(ATRIAL FIBRILLATION) UNAELEWA NINI?


Tatizo la umeme wa Moyo ni pale ambapo  vyumba vya juu vya moyo vinavyohusika na kusukuma damu kunywe moyo (Atria) vinashindwa kufanya kazi sawa sawa kupelekea kushindwa kushirikiana na vyumba viingine vya chini (Ventricle) kuisukuma damu kuingia na  kutoka kwenye moyo kwenda sehemu ziingine za mwili.


Umeme wenyewe wa moyo ni pale ambako moyo wenyewe unazalisha nguvu(umeme) itakayosaidia hivi vyumba vyake kusukuma damu. Umeme huu uzalishwa na seli ambazo hupatika katika chumba cha juu kulia(Right atrium).


 DALILI ZA TATIZO LA UMEME WA MOYO

Mtu anapopata tatizo hili mapigo yake ya moyo huenda kasi sana kufikia mapigo100 hadi 175 kwa dakika,Maumivu ya kifua sehemu ya kulia, kuishiwa pumzi na kuchoka mwili mzima.


NINI VISABABISHI VYA TATIZO 

Visababishi vya tatizo hili viko vingi vikiwemo mtu kuzaliwa na matatizo ya moyo kutofanya kazi vizuri, Shinikizo la damu, kama mtu alishawahi kufanyiwa upasuaji wa moyo, moyo kupata maambukizi, Umri kua mkubwa moyo kufifia uwezo wake wa kufanya kazi nk.


Via afyasolution




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!