UMUHIMU WA KUFANYA CHECKUP MARA KWA MARA

 CHECKUP

• • • • •

UMUHIMU WA KUFANYA CHECKUP MARA KWA MARA 


Kwanza katika swala la watu kwenda hosptal kwa ajili ya afya zao, Wanaume wapo nyuma sana zaidi ya wanawake. Na ukweli ni kwamba sio kwamba hawaumwagi, japo ndyo picha ipo hivo.


Kufanya checkup mara kwa mara sio mpaka ukiwa unaumwa au unahisi dalili ya ugonjwa flani, hapana huweza kuwa kitu endelevu.


UMUHIMU WA KUFANYA CHECKUP MARA KWA MARA 


- Ukiwa na tabia ya kufanya checkup mara kwa mara hukusaidia wewe katika kugundua magonjwa mapema na kupata matibabu.


 Mfano kwa ugonjwa kama Kansa ya matiti, Kansa ya kizazi N.K huweza kutibika kabsa endapo mtu atagundulika mapema na kuanza tiba kabla ya kufikia hatua au stage mbaya kama vile stage 4 ambayo ni ngumu mtu kupona


- Husaidia kwa mtu ambaye amepata ugonjwa ambayo huwa unachelewa kuonyesha dalili ukiwa katika hatua za awali. Mtu huyu huweza kugundua ugonjwa mapema hata kabla ya kuonyesha dalili zozote


- Husaidia mtu kupata tiba sahihi zaidi endapo ana tatizo lolote la kiafya kwenye mwili wake


- Lakini pia hukusaidia wewe kujua afya yako ilivyo kila siku, pamoja na maendeleo yake



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!