USIKIMBILIE DAWA BAADA YA KUONA UNA MIMBA CHANGA ALAFU KUNA VIDAMU DAMU VINATOKA(Waone Wataalam wa Afya)

MIMBA CHANGA

• • • • • •

USIKIMBILIE DAWA BAADA YA KUONA UNA MIMBA CHANGA ALAFU KUNA VIDAMU DAMU VINATOKA(Waone Wataalam wa Afya)


Kuna wanawake hupatwa na hali hii ya kutokwa na vidamu damu katika sehemu za siri wakati wa ujauzito ukiwa mdogo kabsa, hapa tunazungumzia katika wiki za mwanzoni kabla ya Ujauzito kumaliza miezi mitatu ya mwanzoni. Hali hii inaweza kutokea kwa asilimia 20% ya Wanawake baada ya kubeba mimba


ANGALIZO; Damu hiyo ambayo huweza kutoka kipindi cha wiki za mwanzoni mwa ujauzito isiwe nyingi, na wala isichukue mda mrefu. Endapo ikiwa hivo(nyingi na imechukua zaidi ya siku 3) basi kuna tatizo.


Mwanamke hupata mabadiliko mengi katika mwili wake baada ya kubeba mimba na sababu kuu ikiwa ni kutokana na mabadiliko ya vichocheo vyake vya mwilini. 


CHANZO CHA MWANAMKE KUPATA HALI YA KUTOKWA NA VIDAMU DAMU UJAUZITO UKIWA MDOGO SANA


- Hali hii ya Mwanamke kutokwa na vidamu damu wakati wa mimba changa huweza kutokea kipindi cha Yai lililorutubishwa kujishikiza katika ukuta wa Mji wa mimba ambapo kwa kitaalam tunaita Implantation bleeding.


- Sababu nyingine ni mabadiliko ya Mlango wa uzazi au CERVICAL CHANGES baada ya mwanamke kubeba mimba, ambapo mabadiliko haya huhusisha kiwango kikubwa cha damu kuflow na kuja katika eneo hili la mlango wa uzazi au Cervix. Hivo basi baada ya mwanamke kufanyiwa vipimo mbali mbali ambavyo hugusa mlango wa uzazi(Cervix) kama Pap-Test, au Mwanamke kufanya tendo la Ndoa, huweza kusababisha mwanamke kutokwa na vidamu damu kidogo na baadae vikakata.


- Maambukizi ya magonjwa yanayohusisha uke pamoja na Mlango wa uzazi, Hapa tunazungumzia magonjwa mbali mbali ya zinaa kama Kisonono, Chlamydia, Herpes N.K huweza kusababisha hali hii ya mwanamke kupata hali ya vidamu vidamu wakati wa wiki za mwanzoni za ujauzito


- Lakini pia tafiti zinaonyesha kuna baadhi ya Wanawake huendelea kuona siku zao za hedhi hata baada ya kubeba mimba katika wiki za mwanzoni (kabla ya Wiki 12), Japo hedhi hii haiwi kama hedhi ile ya Siku zote


MAMBO YA KUEPUKA UKIWA MJAMZITO


• Epuka kutumia dawa kiholela pasipo maelekezo ya kina kutoka kwa wataalam wa afya


• Epuka kuvaa Nguo za kubana sana tumbo,Mikanda, N.K


• Epuka kuvaa viatu virefu sana,kwani mbali na madhara kama kupata maumivu ya kiuno,mgongo,miguu, kwenye Misuli N.K, Pia unaweza ukadondoka na kuhatarisha ujauzito wako


• Epuka kulalia Mgongo kwani huweza kusababisha Mgandamizo wa mshipa mkubwa wa Damu maarufu kama Inferior Vena Cava na kuleta madhara kwako na kwa mtoto. Unashauriwa kulalia ubavu,hasa hasa ubavu wako wa kushoto.


• Epuka kula udongo wakati wa ujauzito


• Zingatia lishe bora


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LA KIAFYA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!