Ticker

6/recent/ticker-posts

UVUTAJI WA SIGARA HUPUNGUZA NGUVU ZA KIUME(pamoja na hamu ya tendo la ndoa)



 NGUVU ZA KIUME

• • • • •

UVUTAJI WA SIGARA HUPUNGUZA NGUVU ZA KIUME(pamoja na hamu ya tendo la ndoa)


Moja ya madhara makubwa ya uvutaji wa sigara ni pamoja na kupunguza hamu ya tendo la ndoa kwa wote(wanaume na wanawake). 


Uvutaji wa sigara kwa wanaume hupunguza hamu ya tendo la ndoa kwa kupunguza kiwango cha uzalishaji wa vichocheo aina ya testerone mwilini, hivo kumfanya mwanaume asiwe na hamu ya tendo la ndoa.


Pia madhara mengine ya uvutaji wa sigara kwa Wanaume ni kupunguza nguvu za kiume. Hii ni kutokana na kwamba uvutaji wa sigara huathiri mzunguko mzima wa damu katika uume,hivo kuufanya uume ushindwe kusimama vizuri na kufanya kazi kama kawaida.


Pia sigara huathiri utengenezaji wa mbegu za kiume pamoja na uzito wa mbegu,hivo kumuweka mwanaume mvutaji kwenye hatari ya kushindwa kumpa mwanamke mimba.


Uvutaji wa sigara unahusishwa na kuharibu shape ya mbegu za kiume,hivo kusababisha mbegu nyingi kufa.


Pia uvutaji wa sigara huhusika na kuharibu vishipa vidogo ambavyo mbegu hutengenezwa na kupita hapo,hivo kuendelea kusababisha tatizo la mbegu chache kupita.




KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.







Post a Comment

0 Comments