VITU AMBAVYO HURUHUSIWI KUVIFANYA WAKATI UNANYONYESHA MTOTO(kwa lugha nyingine tunasema Don'ts)
KUNYONYESHA
• • • • •
VITU AMBAVYO HURUHUSIWI KUVIFANYA WAKATI UNANYONYESHA MTOTO(kwa lugha nyingine tunasema Don'ts)
Kama nilivyoeleza kwenye makala zangu nyingi zilizopita kwamba, unyonyeshaji ni kuanzita mtoto anapozaliwa mpaka anapofikisha umri wa miaka 2 au 3, huku ikitanguliwa na miezi 6 ya mwanzoni ya kunyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee bila kuchanganyiwa na kitu kingine chochote, kwa kitaalam tunaita EXCLUSIVE BREASTFEEDING.
VITU AMBAVYO HURUHUSIWI KUVIFANYA WAKATI UNANYONYESHA MTOTO(DON'TS)
1. Usianze kumnyonyesha mtoto kabla ya kunawa mikono yako kwa maji safi na sabuni ikiwemo kusafisha chuchu pamoja na maziwa yako.
2. Usimnyonyeshe mtoto ikiwa chuchu yako haijaingia kwenye mdomo wa mtoto na kufunika vizuri(eneo jeusi la titi). Kitendo hiki huweza kusababisha mtoto kunyonya maziwa pamoja na hewa,hivo kumsababishia hewa kujaa tumboni,hali ambayo itamfanya mtoto apate shida na kulia mara kwa mara.
3. Usimnyonyeshe mtoto kwa njia ya mkasi
4. Usimnyonyeshe mtoto ukiwa umekunja miguu yako(wengine huita kukunja 4)
5. Usimnyonyeshe mtoto pamoja na kumpa maji,kwani maziwa ya mama yana kila kitu;
Maziwa ya mama yamegawanyika katika sehemu kuu tatu.
(1) Kuna maziwa ya mwanzo ambayo hukata kiu ya mtoto kabsa kama maji
(2) Kuna maziwa ya katikati ambayo ni mepesi
(3) Na kuna maziwa ya mwisho ambayo ni mazito na haya ndyo mtoto anatakiwa kukutana nayo ili ashibe vizuri.
Kitendo cha kumnyonyesha mtoto kwa muda mfupi husababisha mtoto kushindwa kufikia maziwa haya mazito ambayo ndyo humshibisha mtoto. Ndyo maana unashauriwa kumnyonyesha mtoto kwa muda wa kutosha.
6. Usimpe chakula mtoto ambaye ana umri wa chini ya miezi sita. huyu ananyonya maziwa ya mama peke yake
7. Usikamue maziwa yako ukayaweka halafu baada ya muda ndyo unampa mtoto hapa nazungumzia maziwa yakikaa muda mrefu mfano; baada ya saa 6, usimpe mtoto wako
8. Usimnyonyeshe mtoto ukiwa umelala
9. Usiache kumnyonyesha mtoto maziwa hata kama umeanza kumchanganyia na vitu vingine kwa kipindi cha miaka 2 au 3
10. Usimnyonyeshe mtoto akiwa amelala. Muache aamke kwanza
KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!