UZITO KWA MTOTO
• • • • • •
WASTANI WA ONGEZEKO LA UZITO KWA MTOTO(uzito unaotakiwa kwa watoto)
1. Uzito ambao ni mzuri kwa mtoto ambaye ndyo kazaliwa ni 2.5 mpaka 3.5 kgs
2. Mtoto akiwa na umri wa miezi mitano mpaka sita ; anatakiwa kuwa na uzito mara mbili wa ule ambao kazaliwa nao Mfano; kama kazaliwa na Kg 3 basi ni 3×2= 6 Kgs
3. Mtoto akiwa na umri wa mwaka mmoja uzito unatakiwa kuwa mara tatu ya ule aliyozaliwa nao mfano; kama kazaliwa na kg 3 ni 3× 3= 9 kgs
4. Mtoto akiwa na umri wa miaka miwili uzito unatakiwa kuwa mara nne ya ule aliyozaliwa nao mfano; kama kazaliwa na kg 3 ni 3× 4= 12 kgs
KUMBUKA; wastani wa uzito kwa mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja ni 10kg na wastani wa uzito kwa mtoto mwenye umri wa miaka miwili ni 12 kgs.
5. Lakini pia katika miezi sita ya mwanzoni,mtoto hutakiwa kuongezeka uzito kwa kiwango cha 20 mpaka 30 g kwa siku
6. Ongezeko la 15 mpaka 20g kwa siku kwa kipindi cha miezi sita iliyobakia ili kutumiza mwaka mmoja
7. Huku ongezeko la mwezi,likiwa si chini ya 600g kwa miezi 6 ya mwanzo na 500g kwa miezi 6 iliyobaki kutimiza mwaka 1
#afyaclass #drtareeq
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!