YAJUE MAGONJWA AMBAYO HUWASUMBUA SANA WANAUME

 WANAUME

• • • •

YAJUE MAGONJWA AMBAYO HUWASUMBUA SANA WANAUME


Katika makala hii tunaangalia list au orodha ya baadhi ya magonjwa ambayo huwasumbua sana wanaume wa umri wowote. Kumbuka; namba hizi hazimaanishi chochote, kwamba namba moja ndyo unaongoza,lahasha! hizi ni namba tu,cha msingi ujue baadhi ya magonjwa ambago huwatesa zaidi wanaume, Na magonjwa hayo ni pamoja na;


1. Ugonjwa wa kujaa maji kwenye Korodani ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Hydrocele, Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na mwanaume kuonekana na uvimbe au kuvimba korodani zake.


2. Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu ndani ya korodani ambapo kwa kitaalam huitwa Varicose vein, ambapo pia huambatana na maumivu makali kwa Mgonjwa.


3. Ugonjwa wa tezi dume au Kansa ya Tezi dume, Ugonjwa huu huwatesa wanaume wengi hata kufikia hatua ya kusababisha vifo.


4. Tatizo la Low sperm count, hapa tunazungumzia ile hali ya mwanaume kuzalisha mbegu za kiume chache au chini ya kiwango hata kufikia hatua ya kushindwa kumpa mwanamke mimba au Ujauzito.


5. Tatizo la mwanaume kukosa Nguvu za kiume au kuwa na upungufu wa nguvu za kiume.


6. Matatizo ya akili,Tafiti zinaonyesha kwamba wanaume wengi hushambuliwa na magonjwa ya akili kwa asilimia kubwa zaidi ya Wanawake.


7. Lakini pia Ugonjwa wa UTI AU urinary track infection,maambukizi katika mfumo wa Mkojo, japokuwa wanawake ndyo waathirika wa kubwa wa tatizo hili ila hata wanaume pia huumwa sana ugonjwa wa UTI.


8. Ugonjwa wa fangasi sehemu za siri,maeneo ya uume,ngozi yote inayotenganisha njia ya haja kubwa na uume pamoja na Eneo la Korodani. Ingawa pia fangasi wa sehemu za siri(Candida Albicans) husumbua wanawake zaidi ya wanaume.


9. Magonjwa mbali mbali ya zinaa ikiwemo Ugonjwa wa Chlamydia(kwa asilimia kubwa), Kisonono, kaswende na UKIMWI

N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!