ZIFAHAMU IMANI POTOFU KUHUSIANA NA UKIMWI

 UKIMWI

• • • • •

ZIFAHAMU IMANI POTOFU KUHUSIANA NA UKIMWI


Utangulizi;

• Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini ambao kwa kitaalam hujulikana kama Aquired Immuno deficiency Syndrome au kwa kifupi AIDS.


• Upungufu huu wa kinga mwilini husababishwa na Virusi(VVU-Virusi vya Ukimwi)  ambavyo kwa kitaalam hujulikana kama Human immunodeficiency Virus au kwa kifupi HIV.


IMANI POTOFU KUHUSIANA NA UKIMWI NI PAMOJA NA;


1. Mtu huweza kuambukizwa ukimwi kwa kushikana mikono na muathirika wa ukimwi


2. Mtu huweza kuambukizwa ukimwi kwa kukaa karibu na mtu mwenye virusi vya ukimwi


3. Mtu huweza kuambukizwa virusi vya ukimwi kwa kukumbatiana na muathirika wa Ukimwi


4. Mtu huweza kupata maambukizi ya ukimwi kwa kung'atwa na mbu


5. Mtu huweza kupata maambukizi ya ukimwi kwa kushare Choo au vyombo vya chakula na muathirika wa ukimwi


6. Mtu huweza kupata maambukizi ya ukimwi kwa kuogelea au kuoga sehemu ambapo muathirika wa ukimwi kaoga


7. Mtu huweza kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kukaa sehemu ambapo mauthirika wa ukimwi kakaa


8. Mtu huweza kupata virusi vya ukimwi kwa kushare taulo la kuogea na muathirika wa ukimwi


9. Mtu huweza kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kuvaa nguo za muathirika wa ukimwi


10. Mtu mwenye maambukizi ya ukimwi hawezi kubeba mimba na kuzaa mtoto


11. Kupata maambukizi ya ukimwi ndyo mwisho wa Maisha yako. Lahasha! Kuna maisha baada ya maambukizi ya Virusi vya ukimwi



NB; Hizo zote ni imani potofu na unyanyapaa mkubwa kwa watu wenye Virusi vya ukimwi, epuka kuwa miongoni mwa watu wanaowanyanyapaa waathirika wa ukimwi,ndyo mana nakuelimisha ili uelewe vizuri tatizo hili.


MTU HUWEZA KUPATA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KWA NJIA KAMA HIZI;


• Kuchangia vifaa vyenye ncha kali pamoja na muathirika wa virusi vya ukimwi,na vifaa hivo ni kama; Sindano,Nyembe, pin,N.K


• Kufanya mapenzi bila kutumia kinga au Ngono zembe kwa lugha nyingine


• Watu ambao wanafanya mapenzi kinyume na maumbile wapo kwenye hatari zaidi ya kupata Virusi vya ukimwi


• Unaweza kupata virusi vya ukimwi kwa kuchangiwa damu ya mtu ambaye tayari ameathirika


WATU WALIOPO KWENYE HATARI YA KUPATA VIRUSI VYA UKIMWI(VVU)


- Watumiaji wa madawa ya kulevyia hasa hasa dawa za kujidunga


- Wanaofanya Ngono zembe au wanaofanya mapenzi bila kinga


- Watu ambapo wana wapenzi wengi


- Watu wanaofanya mapenzi kinyume na maambile



KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!