KULALA UCHI
• • • • • •
ZIJUE FAIDA ZA KULALA UCHI AU BILA NGUO
Je wajua faida za kulala uchi au bila nguo?
Bila shaka utashangaa,na wala hujawahi kuwaza kwamba kuna faida za Mtu akilala uchi au kwa lugha nyingine bila nguo.
Wengine wanalala bila nguo kwa kusema ni mazoea yao tu,hawawezi kulala na nguo,lakini bila shaka hata wao hawajui kwamba kuna faida nyingi za kulala bila Nguo.
FAIDA ZA KULALA UCHI AU BILA NGUO NI PAMOJA NA;
- Faida katika kubalance uzito wa mwili, Watu wengi hawajui kwamba ukiwa umevaa nguo huku umelala, mwili huongeza matumizi ya akili katika kufikiria pamoja na hali ya kutokulia kwa mwili au mwili kushindwa kurelax hivo mtu kupata msongo wa mawazo bila yeye kujua wakati amelala,
hali hii humfanya mtu apate njaa sanaa, na kupelekea ulaji wa chakula kuongezeka sana, mwisho wa siku huweza kuwa na tatizo la uzito mkubwa.
- Husaidia katika ulinzi wa Sehemu za siri(kwa Mwanamke na Mwanaume), Endapo mwanamke atalala bila nguo,huweza kuruhusu kiwango kikubwa na chakutosha cha hewa aina ya Oxygen kupenya sehemu za siri na kusaidia kuzuia magonjwa mbali mbali kama vile; Mashambulizi ya fangasi wa ukeni.
Na kwa mwanaume,akilala uchi au bila nguo,husaidia Korodani zake kuwa wazi na kutokupata joto sana,hali ambayo husaidia sana katika afya ya korodani pamoja na utengenezaji wa Mbegu za kiume,
hivo kumuepusha mwanaume na matatizo mbali mbali kama vile; ya kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za Kiume au kwa kitaalam tunaita LOW SPERM COUNT.
- Mtu kulala vizuri, Ni dhahiri kwamba ukilala bila Nguo mwili unakuwa huru sana au una relax hali hii hukufanya ulale vizuri bila kuwa na usumbufu wowote pamoja na kuwa na usingizi wa kutosha.
- Kukulinda dhidi ya magonjwa mbali mbali, hapa tunazungumzia hali ya joto la mwili kushuka kitu ambacho inakuwa vigumu kwa vimelea vya magonjwa mbali mbali kuweza kushambulia mwili wako kwa Urahisi.
- Ukilala bila nguo huufanya mwili pamoja na Vichocheo vya mwili au kwa kitaalam Hormones vifanye kazi kwa urahisi zaidi na kuwa na mazingira mazuri ya kiutendaji kazi tofauti na ukiwa umevaa Nguo wakati wa kulala.
- Kukuepusha na hali ya kuweweseka na kuota ndoto nyingi usku, Hii hali hutokea hasa hasa kwa wale ambao huvaa nguo nzito sana,nyingi na za kubana mwili wakati wa kulala,
hali hii huweza kukufanya ukaota mandoto mengi na kuweweseka wakati wa usku ukiwa umelala.
- Na kwa wale ambao wapo kwenye mahusiano,kulala bila nguo huweza kuimarisha uhusiano, kupunguza kama sio kuondoa kabsa Msongo wa mawazo,kuleta uhuru pamoja na Furaha wakati wa kulala.
KUMBUKA; Hata kwa kipindi cha baridi wataalam wa afya wanashauri bora uwe umejifunika shuka nyingi,nzito au mablangeti mengi kuliko kulala ukiwa umevaa nguo.
ANGALIZO; Kama una matatizo ya kiafya ambayo hayapatani kabsa na hali ya ubaridi, kama matatizo ya vifua,Pneumonia N.K,
Hakakisha unaongea na wataalam wa afya ili wakushauri njia salama kwako na jinsi ya kulala wakati wa Usku.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!