AINA YA MAUMIVU YA KICHWA AMBAYO HUAMBATANA NA HALI YA KUPOOZA UPANDE MMOJA(Hemiplegic migraine)

 MAUMIVU YA KICHWA

• • • •

AINA YA MAUMIVU YA KICHWA AMBAYO HUAMBATANA NA HALI YA KUPOOZA UPANDE MMOJA(Hemiplegic migraine)


Tatizo hili na mtu kupatwa na maumivu makali ya kichwa ambayo huambatana na hali ya kupooza upande mmoja wa mwili wake hutokea mara chache sana, ila lipo na kwa kitaalam linajulikana kama Hemiplegic migraine


DALILI ZA TATIZO HILI LA HEMIPLEGIC MIGRAINE NI PAMOJA NA;


- Mtu kuona marue rue


- Mtu kupata maumivu makali ya kichwa kwa mbele au eneo la paji la usoni


- Mtu kupatwa na kizunguzungu hasa kukiwa na mwanga mkali


- Kupooza sehemu moja ya mwili kama vile mkono,mguu,mdomo n.k


- Mtu kupata shida ya kuongea vizuri


- Mtu kudondoka na kupoteza fahamu


- Mtu kuanza kupoteza kumbukumbu


- Mtu kuwa na dalili zote za kuchanganyikiwa

n.k


CHANZO CHA TATIZO HILI


Zipo baadhi ya sababu ambazo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo hili la maumivu makali ya kichwa ambayo huambatana na mwili kupooza upande mmoja na sababu hizo ni kama vile;


- Kurithi kwa vinasaba vya shida hii kwenye familia au ukoo flani


- Kuwa na tatizo la msongo wa mawazo kwa muda mrefu


- Kukaa kwenye mwanga mkali sana kwa muda mrefu


- Kuwa na shida ya kihisia


- Kukaa kwa muda mrefu bila kulala au kukosa muda wa kutosha wa kulala


- Au kulala sana kwa muda mrefu kuliko kawaida


- Kula sana vyakula vyenye chumvi nyingi


- Matumizi ya pombe kupita kiasi


- Matumizi ya vinywaji vywenye kiwango kikubwa cha Caffeine


- Kukaa kwa muda mrefu bila kula chakula


- Mabadiliko ya gafla ya kimazingira

n.k


MATIBABU YA TATIZO HILI


Matibabu ya tatizo hili huhusisha njia mbali mbali kama vile;


✓ matumizi ya dawa jamii ya Beta blockers


✓ Mtu kupata drip au kupitishiwa dawa kwanjia ya mshipa yaani IV kama vile magnessium


✓ Matumizi ya dawa jamii ya non-steroidal antiinflammatory drugs


✓ matumizi ya dawa kama vile Verapamil


✓ Pamoja na kuepuka tabia hatarishi zote ambazo huweza kuongeza ukubwa wa tatizo


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!