MGONGO
• • • • •
AINA YA MAUMIVU YA MGONGO AMBAYO LAZIMA UMUONE DACTARI(soma)
Maumivu ya mgongo kwa watu imekuwa ni jambo la mara kwa mara huku maumivu hayo yakihusishwa na sababu mbali mbali kama vile;
- kufanya kazi za kuinama sana kwa muda mrefu
- Kufanya kazi ngumu sana
- Maambukizi ya magonjwa mbali mbali kama homa ya Uti wa mgongo n.k
Huku baadhi ya watu wakitumia tu dawa nyumbani na tatizo la mgongo kuisha
Lakini kuna aina ya maumivu ya mgongo ambayo lazima kukutana na wataalam wa afya kwa ajili ya uchunguzi zaidi na tiba sahihi baada ya vipimo.
AINA YA MAUMIVU YA MGONGO AMBAYO LAZIMA UMUONE DACTARI
1. Maumivu ya mgongo ambayo huambatana na kupungua sana kwa uzito wako wa mwili
2. Maumivu ya mgongo ambayo huambatana na kushindwa kutembea kabsa
3. Maumivu ya mgongo ambayo hudumu kwa zaidi ya wiki moja kila siku mfululizo
4. Maumivu ya mgongo ambayo hayapungui wala kuisha licha ya kupata muda wa kutosha wa kupumzika na kulala kitandani
5. Maumivu ya mgongo ambayo huambatana na miguu kuchoma au kuwaka moto
6. Maumivu ya mgongo ambayo huambatana na kukosa pumzi au kushindwa kupumua
Kwa dalili hizi za maumivu ya mgongo kutana mara moja na wataalam wa afya kwa ajili ya msaada zaidi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!