CHANZO CHA MAUMIVU MAKALI YA TUMBO WAKATI WA KUKOJOA

 TUMBO

• • • •

CHANZO CHA MAUMIVU MAKALI YA TUMBO WAKATI WA KUKOJOA


Maumivu makali ya tumbo huweza kutokea wakati wa kukojoa hasa kwa wanawake ikilinganishwa na wanaume,Na kuna sababu zaidi ya moja ambayo huweza kusababisha hali hii.


Maumivu haya yanaweza kuwa ya aina mbali mbali kama vile; tumbo kuchoma kama kuna mtu anachoma na kitu chenye ncha kali, maumivu ya tumbo kama kuna mtu anakukata na kisu, na wengine hupata maumivu upande mmoja hasa wa kushoto karibu na kitovu kwa chini kidogo.


CHANZO CHA MAUMIVU MAKALI YA TUMBO WAKATI WA KUKOJOA


Sababu za maumivu makali ya tumbo wakati wa kukojoa ni kama zifuatavyo;


1. Kuwa na maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo yaani Urinary track infection au UTI


2. Kuwa na tatizo la mawe kwenye figo ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Kidney stones


3. Kuwa na tatizo la uvimbe kwenye ukuta wa ndani wa uzazi kwa mwanamke yaani kwa kitaalam Endometriosis


4. Kuwa na tatizo kwenye tezi dume ikiwa ni pamoja na uvimbe,kansa N.k


5. Kuwa na tatizo la kutokewa na kitu kama kifuko kwenye njia ya mkojo yaani urethral Diverticulum

n.k


Hivo ukiwa na tatizo la maumivu makali ya tumbo wakati wa kukojoa ongea na wataalam wa afya ili upate vipimo pamoja na tiba sahihi kwako.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!