ULIMI
• • • •
CHANZO CHA MAUMIVU MAKALI YA ULIMI
Kwa namna moja au nyingine mtu huweza kupata maumivu makali kwenye ulimi wake bila kujua sababu hasa ni nini, hali hii huweza kumsababisha ashindwe kula chakula, kukosa furaha n..k
SABABU AMBAZO HUWEZA KUWA CHANZO CHA MAUMIVU YA KWENYE ULIMI
Baadhi ya sababu katika makala hii kwa namna moja au nyingine huweza kuwa chanzo cha maumivu ya Ulimi wako
• Tatizo la maambukizi ya Fangasi, hapa nazungumzia fangasi wa Ulimi. Hali hii huweza kuwa chanzo cha ulimi kuchubuka,kuwa na vidonda pamoja na maumivu makali ya Ulimi.
• Maumivu ya Ulimi huweza kuchangiwa na ajali mbali mbali ikiwa ni pamoja na Mtu kung'atwa ulimi au kujing'ata mwenyewe,kuchomwa na kitu cha ncha kali n.k
• Mtu kuwa na tatizo la Kansa ya kwenye Ulimi
• Urembo mbali mbali kama vile urembo wa kuvaa vidani kwenye ulimi n.k
• Mtu kushambuliwa na virusi jamii ya Herpes
• Kuwa na shida kwenye mfumo wa fahamu au Nerves
• N.k
Endapo una tatizo hili kutana na wataalam wa afya kwa Ajili ya uchunguzi zaidi na kupata tiba sahihi
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!