MAZIWA
• • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA KUHARISHA,TUMBO KUJAA GESI BAADA YA KUNYWA MAZIWA
Kuna baadhi ya watu baada ya kunywa maziwa au kula vitu vyovyote ambavyo vina products za maziwa ndani yake huanza kupata madhara mbali mbali kama vile;
- Tumbo kujaa gesi sana
- Tumbo kuuma sana
- Tumbo kunguruma sana
- Kutapika sana
- Au kuharisha sana
Je tatizo hili husababishwa na nini? chanzo chake ni kipi?
CHANZO CHA TATIZO HILI
✓ Kutokana na tafiti mbali mbali za kitaalam,shida hii ambayo hutokea baada ya mtu kunywa maziwa au kula vitu vyenye maziwa ndani yake hutokana na Mfumo wa umeng'enyaji kushindwa kumeng'enya Lactose.
Hali hii hutokana na utumbo mdogo kushindwa kuzalisha vimeng'enyaji vya kutosha yaani enzymes ambao wanajulikana kwa jina la LACTASE ambao ndyo huhusika na kumeng'enya sukari iliyopo kwenye maziwa yaani Milk Lactose.
MATIBABU YA TATIZO HILI
Matibabu ya tatizo hili Huhusisha matumizi ya dawa mbali mbali pamoja na mgonjwa kupunguza au kuacha kutumia maziwa au vitu vyenye maziwa ndani yake ndani ya angalau mwezi au miezi kadhaa wakati akiwa kwenye tiba.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!