CHANZO CHA TATIZO LA KUSHINDWA KUZUIA MKOJO(urinary incontinence)

 MKOJO

• • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA KUSHINDWA KUZUIA MKOJO(urinary incontinence)


Hili ni tatizo ambalo huhusisha mtu kushindwa kuzuia mkojo,hivo kupelekea mkojo kutoka wenyewe, mtu kujikojolea N.k


Tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama Urinary incontinence, na zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuhusishwa na uwepo wa tatizo hili.


CHANZO CHA TATIZO LA KUSHINDWA KUZUIA MKOJO(urinary incontinence)


- Misuli ya Kibofu cha mkojo kupoteza uwezo wake wa kiutendaji na kushindwa kuzuia mkojo kutoka hasa kibofu cha mkojo kikijaa


- Maambukizi ya magonjwa mbali mbali kwenye mfumo mzima wa njia ya mkojo kama vile UTI sugu


- Tatizo la mabadiliko ya vichocheo vyako vya mwilini


- Matumizi ya vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha Caffeine


- Matumizi ya kiwango kikubwa cha carbonate


- Unywaji wa pombe kupita kiasi


- Uvutaji wa sigara


- Tatizo la kuwa mnene au na uzito kupita kiasi


- Matumizi ya vitu kama baadhi ya virutubisho ambavyo hutoa kiwango kikubwa sana cha vitamin C mwilini


- Matumizi ya baadhi ya dawa ambazo huweza kuleta athari kwenye mfumo mzima wa mkojo


- Hali ya kuwa mjamzito huweza kupelekea mama kupoteza uwezo wa kuzuia mkojo kutoka


- Tatizo la kuwa na saratani ya kibofu


DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


✓ Mtu kujikojolea baada ya kucheka sana


✓ Mtu kujikojolea baada ya kupiga chafya


✓ Mtu kujikojolea baada ya kukohoa kwa nguvu


✓ Mtu kujikojolea wakati anafanya mazoezi ya mwili


✓ Mtu kujikojolea baada ya kunyanyua kitu kizito


✓ Mtu kujikojolea wakati amelala


✓ Mtu kujikojolea wakati akiwa na hasira sana

N.K


MATIBABU YA TATIZO HILI


Tiba sahihi ya tatizo hili hutegemea na chanzo husika.

Kuna matibabu mbali mbali ikiwa ni pamoja na; matumizi ya dawa za kurudisha uwezo wa misuli ya kibofu cha mkojo kufanya kazi, dawa za kudhibiti vichocheo vya mwili,dawa za maambukizi ya UTI, n.k


Pamoja na njia ya mazoezi kwa ajili ya kurudisha uwezo wa mwili kudhibiti mkojo kutoka.


MAMBO YA KUEPUKA ILI KUJIKINGA NA TATIZO HILI;


• epuka matumizi ya pombe kupita kiasi


• epuka matumizi ya sigara


• fanya mazoezi


• epuka unene au uzito kupita kiasi


• epuka matumizi ya vinywaji venye kiwango kikubwa cha caffeine,carbonate n.k



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!