CHANZO CHA TATIZO LA MAUMIVU YA MATITI(dalili na tiba)

 MATITI

• • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA MAUMIVU YA MATITI(dalili na tiba)


Moja ya tatizo ambalo hutokea kwa wanawake wengi ni pamoja na hili la maumivu ya matiti ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Mastalgia.


Tatizo hili la maumivu makali huweza kuhusisha titi moja au matiti yote mawili.


CHANZO CHA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


✓ Maumivu kutokea wakati mwanamke akiwa kwenye siku zake za hedhi


✓ Maumivu kutokea kutokana na mabadiliko ya vichocheo vya mwili


✓ Maumivu kutokana na kuumia,ajali,kuchomwa na kitu cha ncha kali,kuungua N.k


✓ Maumivu kutokana na titi au matiti kuwa na shida ya kansa(saratani) ya matiti


✓ Maumivu kutokana na maambukizi ya bacteria ndani ya titi


✓ Maumivu kutokana na shida ya kutokuwa na uwiano sawa wa Fatty acid yaani kwa kitaalam fatty acid imbalance


✓ Matumizi ya baadhi ya dawa ambazo huhusika moja kwa moja na kuleta mabadiliko kwenye vichocheo vyako vya mwili


✓ Mwanamke ambaye kafanyiwa upasuaji wa titi


✓ Maumivu kutokana na kuziba kwa mishipa ya damu ndani ya titi au matiti

N.K


MATIBABU YA TATIZO HILI LA MAUMIVU YA MATITI


- Matibabu ya tatizo hili la maumivu ya matiti yaani mastalgia ni pamoja na;


 matumizi ya dawa mbali mbali za kukata maumivu,


matumizi ya dawa za kurekebisha kiwango cha hormone mwilini


Upasuaji kwa mtu ambaye ana shida ya kuziba mishipa ya damu ndani ya titi


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!