SHINGO
• • • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA MAUMIVU YA SHINGO(pamoja na tiba yake)
Maumivu makali ya shingo limekuwa tatizo ambalo huwapata watu wengi sana kwa hivi sasa, huku kukiwa na sababu mbali mbali ambazo huhusishwa na uwepo wa shida hii.
Je chanzo chake kikubwa ni kipi? dalili zake ni zipi? na nini kifanyike kama mtu ana maumivu makali ya shingo?
CHANZO CHA TATIZO LA MAUMIVU YA SHINGO
- Maambukizi ya magonjwa mbali mbali kama vile; Meningitis, kansa N.k
- Kulala vibaya au kukaa vibaya huweza kusababisha maumivu makali ya shingo
- Tatizo la kuharibika kwa nerves mbali mbali maeneo ya shingoni
- Kuumia,kuanguka au kupata ajali yoyote na kugongwa maeneo ya shingoni
- Kubeba vitu vizito sana kichwani au begani
- Kufanya kazi za kuinamisha kichwa kwa muda mrefu kama kusoma
- kutumia vifaa kama computer,simu N.k kwa muda mrefu
- Pia wataalam wa afya huhusisha uvutaji wa sigara na maumivu ya shingo mara kwa mara
DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;
- Mtu kupata maumivu makali ya shingo
- Mtu kushindwa kugeuza shingo au shingo kukaza sana na kuwa ngumu
- Kupata maumivu makali ya kichwa
- Kichwa kuwa kizito sana na kushindwa kusogeza kichwa
MATIBABU YA TATIZO HILI
✓ Matibabu ya tatizo hili hutegeme chanzo chake; hivo kuna njia mbali mbali za kutibu tatizo hili kama vile; mtu kupewa dawa za kutibu magonjwa kama meningitis pamoja na kuepuka vitu mbali mbali kama vile;
1. Kuepuka kuinamisha kichwa kwa muda mrefu mfano wakati wa kusoma n.k
2. Kuepuka kubeba vitu vizito sana kichwani
3. Kuepuka uvutaji wa sigara
4. Kuepuka matumizi ya vifaa kama computer au simu kwa muda mrefu sana
5. Kujitahidi sana kujizoesha kulala bila kujikunja sana shingo n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!