MTOTO
• • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUSAGA MENO
Tatizo la mtoto kusaga au kusigina meno ni tatizo ambalo huwapata baadhi ya watoto, na Tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 20% ya watoto kati ya mwaka Mmoja na miaka Kumi na moja hupatwa na tatizo hili la kusigina meno.
CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUSAGA MENO
Zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia hali hii kama vile;
- Mihemko ya usiku pamoja na tatizo la mtoto kukosa usingizi
- Mtoto ambaye anapata shida wakati wa kupumua hali ambayo husababisha mtoto apumue kwa mdomo
- Mtoto kuwa na tatizo la kuvimba kwenye tezi
- Mtoto kupatwa na tatizo la kufunga njia ya hewa wakati akiwa amelala
- Mtoto kuwa na meno ambayo yameota kwa mpangilio mbaya
- Mtoto kuwa na matatizo ya akili,mtindio wa ubongo n.k
- Mtoto kuwa na shida kwenye ungamo la taya na fuvu la kichwa
- Pia hali ya mama kuwa na msongo mkubwa wa mawazo wakati wa ujauzito huweza kupelekea kumzaa mtoto mwenye shida hii
- Hali ya mtoto kuwa na wasiwasi sana na hofu kubwa kila mara
n.k
MATIBABU YA TATIZO HILI
Tatizo hili la mtoto kusaga meno hupona lenyewe bila matibabu, lakini endapo hali imekuwa mbaya zaidi kutana na wataalam wa Afya hasa wanaohusiana na magonjwa ya watoto pamoja na meno.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!