CHANZO CHA TATIZO LA MWANAUME KUCHELEWA KUFIKA KILELENI(wakati wa tendo la ndoa)
WANAUME
• • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA MWANAUME KUCHELEWA KUFIKA KILELENI WAKATI WA TENDO LA NDOA
Tatizo hili la mwanaume kuchelewa kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa huweza kutokea gafla na kuisha lenyewe au kuwa ni tatizo la muda mrefu.
je nini chanzo kikubwa cha tatizo hili?
CHANZO CHA TATIZO LA MWANAUME KUCHELEWA KUFIKA KILELENI WAKATI WA TENDO LA NDOA
Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mwanaume kuchelewa kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa kama vile;
- Mwanaume kuwa na msongo wa mawazo wakati anashiriki tendo la ndoa
- Mwanaume kutokuwa na hamu kabsa ya kufanya mapenzi
- Mwanaume kuwa na tatizo linalosababisha mbegu za kiume kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala kutoka nje kwa kitaalam hujulikana kama Retrograde ejaculation
- Tatizo la mvurugiko wa vichocheo vyake vya mwilini hasa hasa kichocheo aina ya Testosterone.
- Mwanaume kuwa na hofu kuu pamoja na wasiwasi wakati anashiriki tendo la ndoa
- Mwanaume kusumbuliwa na magonjwa ya akili
- Matumizi ya baadhi ya dawa
- Matumizi ya pombe kwa mwanaume kupita kiasi
- Mwanaume kupata ajali na kuumia sehumu za siri
- Kuharibiwa kwa mfumo wa fahamu(nerves) ambazo huhusika moja kwa moja na mwanaume kufika kileleni
- Mwanaume kuwahi kufanyiwa upasuaji sehemu za siri
- Mwanaume kuzaliwa na madhaifu kwenye mfumo wake wa uzazi
- Mwanaume kuwa na maambukizi sugu kwenye mfumo mzima wa mkojo yaani UTI
MATIBABU YA TATIZO HILI
zipo njia mbali mbali ambazo hutumika kumsaidia mwanaume mwenye shida hii kulingana na chanzo cha tatizo lake ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa mbali mbali, kuacha pombe, kuacha baadhi ya dawa pamoja na matibabu ya Psychotherapy.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!