MJAMZITO
• • • • •
DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO(muhimu sana kujua)
Katika maisha ya ujauzito kuna vitu vya muhimu kujua ili kuepuka kupata madhara mbali mbali ndani ya kipindi hiki na moja ya vitu muhimu ni kujua dalili zote za hatari wakati wa ujauzito.
DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO NI PAMOJA NA;
1. Kuvuja damu ukeni wakati wa ujauzito
2. Kutomsikia mtoto akicheza kwa zaidi ya masaa 24 kwa wale ambao ujauzito umefikia umri wa mtoto kucheza tumboni
3. Kuvimba sana miguu,uso pamoja na mikono wakati wa ujauzito
4. Kuona marue rue wakati wa ujauzito
5. Kuumwa sana au kupata maumivu makali ya kichwa wakati wa ujauzito
6. Kuwa na hali ya mwili kutetemeka au kutingishwa
7. Joto la mwili kupanda au kuwa na Homa wakati wa ujauzito
8. Kutoa uchafu wenye harufu mbaya ukeni wakati wa ujauzito
9. Kutoa maji maji yenye harufu mbaya ukeni wakati wa ujauzito
10. Chupa ya uzazi kupasuka au kwa kitaalam tunaita ruptured membrane.
11. Kupatwa na maumivu makali ya tumbo wakati wa ujauzito
12. Kushindwa kupumua kabsa wakati wa ujauzito
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!