DALILI ZA KUPUNGUKIWA NA MAJI MWILINI

 MAJI

• • • •

DALILI ZA KUPUNGUKIWA NA MAJI MWILINI


Moja ya vitu hatari kabsa kwenye mwili wa binadamu ni tatizo la maji ya mwili kupungua sana, tatizo hili linaweza kusababisha kifo ndani ya muda mfupi hata kuliko kuishiwa na damu mwilini.


Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mtu kuishiwa na maji yake ya mwili ikiwa ni pamoja na; Tatizo la kuharisha sana, tatizo la kutapika sana N.K


DALILI ZA KUPUNGUKIWA NA MAJI MWILINI


Zipo dalili mbali mbali za kupungukiwa na maji mwilini ikiwa ni pamoja na;


1. Kukauka sana Mdomo ikiwa ni pamoja na Lips za mdomo


2. Kupatwa uchovu mkali wa mwili


3. Kupata na hali ya usingizi mzito hata kama ni mchana


4. Kukojoa mara chache zaidi kuliko kawaida huku mkojo ukiwa na rangi isiyo ya kawaida mfano njano iliyokolea N.K


5. Mwili kukosa nguvu kabsa na wengine hata kushindwa kusimama au kudondoka chini


6. Macho yako kuingia ndani zaidi kuliko kawaida


7. Kupatwa na hali ya ukakamavu pamoja na ugumu usio wa kawaida kwenye Ngozi yako ya mwili

N.K


MATIBABU YA TATIZO HILI LA KUPUNGUKIWA NA MAJI MWILINI


Ili mgonjwa apone tiba sahihi ni kurudisha kiwango cha maji kilichopotea mwilini kwa kutumia njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na;


 Mgonjwa kuanza dose ya kupewa madrip ya Maji, Kula vyakula vya maji maji sana ikiwa ni pamoja na kula sana matunda kama vile matikiti maji


Na kuhakikisha unakunywa maji si chini ya Lita 3 kwa siku baada ya Dose ya hospitalini


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!