MFUMO WA HEWA
• • • •
DALILI ZA MAAMBUKIZI KWENYE MFUMO WA HEWA(respiratory system)
Yapi magonjwa mengi pamoja na vimelea mbali mbali vya magonjwa ambavyo hushambuliwa mfumo mzima wa hewa ikiwa ni pamoja na Mapafu na vifuko vya hewa maarufu kama Alveoli.
Mfumo mzima wa hewa ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Respiratory system huanzia puani mpaka kwenye mapafu ambapo ndipo kuna vifuko vya hewa ambavyo hujulikana kama Alveoli.
DALILI ZA MAAMBUKIZI KWENYE MFUMO WA HEWA(respiratory system)
Mtu mwenye maambukizi kwenye mfumo wa hewa huweza kupata dalili zifuatazo;
- Kupata hali ya mafua makali mara kwa mara
- Kupata hali ya kikohozi ambapo huweza kuwa kikohozi kikavu au makozi yenye damu, uchafu mweupe au usaha n.k
- Kupata shida ya upumuaji
- Kupata tatizo la maumivu makali ya kifua
- Kuwa na shida ya kukosa hewa au kuishiwa na pumzi
- Kuwa na tatizo la kudondoka na kuzimia
- Mgonjwa kupoteza fahamu
- Mwili kuchoka sana kuliko kawaida
- Kupata maumivu makali ya misuli pamoja na viungo mbali mbali vya mwili
- Kupata kichefuchefu kikali pamoja na kutapika
- Maumivu makali ya kichwa
- Joto la mwili kupanda au mgonjwa kuwa na homa
n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!